Jumatatu, 10 Machi 2014

WAFANYABIASHARA WA MCHANGA NA KOKOTO JIJI LA MBEYA WAJA JUU KUILALAMIKIA WIZAZRA YA NISHATI NA MADINI

 
 

 
 
 
Bwana nidhamu wa wachimbaji na wasafirishaji bidhaa hizo Peter Hezron N’gwavi amesema kuwa kitendo cha tozo na leseni kitafanya vijana waliojiajiri kuanza kufanya vitendo vya uhalifu kutokana na ukosefu wa mitaji.
 

 
 
Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza amesema kuwa madai yao hayahusu ofisi yake bali wenye dhamana ya kujibu kero hizo ni mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Nishati na Madini hivyo atawaomba wawakilishi wao waweze kujibia kero zao.
 
 
 
 Mwanasheria wa jiji akifafanua jambo 
 
Mhandisi wa Jumanne M. Nkana ambaye ni Afisa Mfawidhi ofisi ndogo ya TMAA Mbeya amesema kuwa waraka wa kulipia bidhaa za Mchanga,Kokoto na Mawe ulipitishwa na Bunge Mwaka 2010 ndipo ulipoanza kutumika rasmi kwa tozo la asilimia 3 kwa bei ya bidhaa iliyopo Sokoni.
 
 
 
 
 
 
 
 
Wafanyabiashara ya Madini ya mchanga,kokoto na mawe Jiji la Mbeya wameandamana kwenda ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji kwa kutumia maroli kupinga waraka wa Wizara ya Nishati na Madini unaowataka watumiaji wa bidhaa hiyo kulipia shilingi elfu mbili mia tano kuanzia Machi 3 mwaka huu.

Maandamano hayo yalipokelewa na Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza ofisini kwake ambapo alikana kutoa waraka huo na kufafanua kuwa waraka huo umetolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini[Tanzania Minerals Audit Agency-TMAA].

Akitoa malalamiko yao mbele ya Mkurugenzi Bwana nidhamu wa wachimbaji na wasafirishaji bidhaa hizo Peter Hezron N’gwavi amesema kuwa kitendo cha tozo na leseni kitafanya vijana waliojiajiri kuanza kufanya vitendo vya uhalifu kutokana na ukosefu wa mitaji.

Mkurugenzi wa Jiji amesema kuwa madai yao hayahusu ofisi yake bali wenye dhamana ya kujibu kero hizo ni mamlaka husika ambayo ni Wizara ya Nishati na Madini hivyo atawaomba wawakilishi wao waweze kujibia kero zao.

Mhandisi wa Jumanne Mohammed ambaye ni Afisa Mfawidhi ofisi ndogo ya TMAA Mbeya amesema kuwa waraka wa kulipia bidhaa za Mchanga,Kokoto na Mawe ulipitishwa na Bunge Mwaka 2010 ndipo ulipoanza kutumika rasmi kwa tozo la asilimia 3 kwa bei ya bidhaa iliyopo Sokoni.

Hata hivyo Mohammed amesema kuwa leseni za uchimbaji wa bidhaa za ujenzi hazihusiani na madereva wanaobeba bidhaa  hiyo hivyo wao wanapobeba bidhaa hizo wanapaswa kupata kibali kuoka kwa mmiliki wa mgodi wa madini hayo ambapo kibali hicho hutolewa bure katika ofisi yake iliyopo eneo la Mwanjelwa Jengo la IFAD.

Alimaliza kwa kuwataka wanaotaka kufanya biashara hiyo wafuate taratibu za kisheria ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima kwani hali hiyo inaikosesha Serikali pato halali linalotokana na watu wachache wanaojinufaisha bili kufuata taratibu.
 
endelea kufuatilia blog hii kwa matukio zaidi   
 

SOMA VICHWA VYA MAGAZETI YA LEO HAPA

 

 
 
 
 
 
 

Ijumaa, 7 Machi 2014

HILI NDILO BUNGE LA KATIBA LA TANZANIA

TUKIO KATIKA PICHA: TAZAMA WABUNGE WALIVYOPIGWA BUTWAA JANA KATIKA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Halima Mdee, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), akiwa haamini kinachoendelea kwenye ukumbi wa bunge wakati wajumbe wa bunge hilo walipocharuka jana na hivyo kumlazimisha mwenyekiti wa muda wa bunge hilo Pandu Ameir Kificho, kuliahirisha kwa muda ili kuepusha uchafuzi zaidi wa "Hali ya Hewa"

Halima Mdee akibadilisha style za "mishangao" wakati "Sinema" ya bure ikiendelea

Mbuneg MosesMachali

Christophe Ole Sendeka, naye hakuwa nyuma kwenye "sheshelumbe" la Jana Alhamisi Machi 6, 2014


BUNGE maalum la Katiba, Jana Alhamisi Machi 6, 2014, liligeuka uwanja wa “Mapambano” kama ile vita iliyotikisa ulimwengu, vita ya Kosovo kule eneo la Balkan.

Hata hivyo sio mapambano ya ngumi bali Majibishano makali yalizuka wakati wajumbe wakiendelea kujadili kanuni zitakazokuwa dira ya kuliongoza bunge hilo maalum, ambalo linaketi pale “mjengoni” kwenye ukumbi wa Bunge la Tanzania mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho, alilazimika kuliahirisha bunge hilo kwa takriban masaa manne, baada ya sintofahamu iliyohanikiza ukumbi huo unaochukua takriban watu 700.

Malumbano hayo yalikuwa ni kati ya wajumbe na mwenyekiti wakati mwingine wajumbe kwa wajumbe, picha kadhaa zilizopigwa na waandishi wa habari wakati sakata hilo likiendelea, zinaonyesha, wajumbe kama vile, Christopher Ole Sendeka, Waziri wa sheria na katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamisi Bakari,Moses Machali na wajumbe wengine kadhaa, wakitoa maneno makali dhidi yao wao wenyewe na wakati mwingine wakimtuhumu mzee Kificho kwa upendeleo.

Baadhi ya wajumbe wa bunge hilo, kama Halima Mdee, kuna wakati alionekana akiwa ameshikwa na butwaa asiamini kinachoendelea ukumbini.

Kasheshe hizo zinajiri huku wajumbe hao wakiwa hata kuapishwa bado, na wachambuzi wa mambo wanabashiri kuwa hata mpango wa Ikulu wa kutaka hotuba ya uzinduzi wa bunge hilo kufanyika wiki hii huenda usifanikiwe kwani hata uchaguzi wa mwenyekiti bado kufanyika na kazi ya kuapisha wajumbe hao zaidi ya 600 huenda ikachukua hadi siku tatu.


Hebu muone uyu naye.....

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda(Katikati) na wazito wengine, wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Thomas Kashilila baada ya kutokea kizaa zaa

Wajumbe wa bunge maalum la Katiba, wakitoka ukumbini baada ya kuahirishwa kwa muda kufuatia sintofahamu iliyotokea

Waziri wa Sheria na Katiba wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari..
KAZI IPO KWA KWELI KAMA MAMBO YENYEWE NDIO HAYA

Jumanne, 4 Machi 2014

HUYU NDIYO CHATU ALIYEWEZA KUPIGANA NA KUMSHINDA MAMBA NA KUMMEZA KABISA HIKO AUSTRALIA

 
Nyoka huyo alijipinda kwa Mamba na kumbana hadi akafa
Chatu ameshinda vita vikali dhidi ya Mamba Kaskazini mwa mji wa QueensLand, kupigana na Mamba, kumpinda na kisha kumla.
Tukio hilo lilishuhudiwa katika ziwa Moondarra, karibu na mlima Isa na kunaswa kwa kamera na wakazi wa eneo hilo siku ya Jumapili.
Nyoka huyo mwenye urefu wa futi 10, alijipinda kwa Mamba na kuanza kupambana naye majini.
Hatimaye, Nyoka huyo alifanikiwa kumshinda Mamba na kumtoa nje ya maji na kisha kumla.

Nyoka alimvuta Mamba na kumtoa ndani ya Maji

Chatu huyo alianza kumla Mamba na kushangaza wakazi

Baada ya mlo huo mkubwa Nyoka alijiendea zake
Tiffany Corlis,mkazi wa eneo hilo, alishuhudia pambano hilo na kupiga picha hizi.
"lilikuwa jambo la ajabu sana, '' aliambia BBC
"Tulimuona Nyoka akipambana na Mamba , alifanikiwa kumbana mamba hasa katika sehemu ya miguu ili kumdhibiti.''
"Pambano lilianzia ndani ya maji. Mamba alikuwa anajaribu kuweka kichwa chake juu ya maji wakati mmoja ingawa Nyoka alikuwa amembana sana.''
"Baada ya Mamba kufa Nyoka alijikunjua, na kuja mbele ya Mamba huyo na kuanza kumla,'' alisema Tifanny.
Bwana Corlis alisema kuwa ilimchukua nyoka muda wa robo saa kumla mamba huyo.
''Bila shaka Nyoka huyo alishiba vyema, na hatujui alikokwenda, baada ya mlo wake,'' alisema mama huyo ambaye hakutaka kusuburi kumuona Nyoka tena.
Mtu mwingine aliyeshuhudia pambano hilo Alyce Rosenthal, alisema kuwa wanyama hao wawili walipambana kwa karibu saa 5. Hatimaye wote walionekana wachovu.

ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO ZAIDI