Jumatano, 20 Novemba 2013

HIVI NDIVYO MAUAJI YA WATU YALIVYOTOKEA KATIKA NGOME YA HEZBOLLAR

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115932_blast_afp-1.jpg 
Takriban watu 22 wameripotiwa kufariki katika milipuko miwili ambayo ililenga ubalozi wa Iran mjini Beirut, mji mkuu wa Lebanon
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115934_blast_afp-2.jpg
Afisaa mmoja mkuu katika ubalozi huo Ebrahim Ansari alikuwa miongoni mwa waliofariki. Maafisa wamesema kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115936_blast_ap-3.jpg
Picha nyingi za mashambulizi hayo zilionyesha magari yakiteketea pamoja na miili ya watu ikiwa imetapakaa kwenye barabara za eneo hilo. Majumba pia yaliharibiwa vibaya
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115938_blast_ap-4.jpg
Iran inaunga mkono kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Hezbollah ambalo limewapeleka wapiganaji nchini Syria kuunga mkono serikali ya Rais Bashar al Assad. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115940_blast_afp-5.jpg
Duru zinasema kuwa moja ya milipuko hio, ilisababishwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga, wakati shambulio la pili lilitokana na bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115942_blast_reuters-6.jpg
Shirika la habari la Reuters linanukuu kituo cha televisheni cha CCTV, kikionyesha mwanamume mmoja akikimbia kutoka katika ubalozi wa Iran na kisha kujilipua
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115944_blast_reuters-7.jpg
Balozi wa Iran nchini Beirut alithibitisha kifo cha bwana Ansari, ingawa haijulikani ikiwa alikuwa ndani ya ubalozi au katika jengo jirani 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115946_blast_ap-8.jpg
Syria imelaani vikali mashambulizi hayo. Mgogoro wa kisiasa nchini Syria umechochea kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini Lebanon.