Alhamisi, 24 Oktoba 2013

WANACHAMA WA CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO TAZARA MBEYA WAFANYA MKUTANO WAO WA 20

HIZI NDIZO OFISI ZA CHMA CHA AKIBA NA MIKOPO TAZARA MBEYA
MENEJA WA CHAMA NDUGU PHILEMON KADUMA AKISOMA AJENDA ZA MKUTANO
HAWA NI KAMATI SIMAMIZI YA CHAMA
KUSHOTO NI NDG YUNUS BASHANGE (M/KITI)
KATIKATI NI NDG ROSEMARY KINYAGA (KATIBU) NA
KULIA NI NDG BETHUEL KAGIMBO (MJUMBE)
MEZA YA URATIBU WA MAMBO YA MKUTANO WA CHAMA
 MWAKILISHI KUTOKA OFISI ZA USHIRIKA JIJI LA MBEYA NDG ISACK MPANGALA AKIONGEA NA WANACHAMA
WANACHAMA WAKIFUATILIA KWA MAKINI AJENDA ZA MKUTANO
MOJA YA WAJUMBE WA CHAMA NDUGU ISACK SAGUDA AKICHANGIA HOJA ZA MKUTANO MKUU
MWANDISHI WA HABARI WA STAR TV NDG FREDRICK BAKALEMWA AKICHUKUA MATUKIO YA MKUTANO
AFISA MAHUSIANO CRDB NDUGU MANOTA AKITOA UFAFANUZI JUU YA KUKOPA MIKOPO KWA BUSA KWA WANACHAMA KUTOKA TAASISI ZA FEDHA
BAADHI YA WAJUMBE KUTOKA MATAWI MABLIMBALI YA CHAMA
MHASIBU WA CHAMA NDG ELIKANA KAGOMA AKITOA UFAFANUZI WA HESABU ZA CHAMA KWA WANACHAMA
MWENYEKITI WA KAMATI YA MIKOPO NDG VERAND SWAI AKITOA TAARIFA FUPI KWA WANACHAMA JUU YA MWENENDO WA MIKOPO CHAMANI
MWENYEKITI KAMATI SIMAMIZI NDG YUNUS BASHANGE AKISOMA TAARIFA FUPI YA KAMATI SIMAMIZI KWA WANACHAMA
MKAGUZI MKUU WA HESABU WA NJE NDG YAWAYAWA AKISOMA HESABU ZA CHAMA ZILIZOKAGULIWA MWAKA 2012 AKISOMA TAARIFA YA UKAGUZI KWA WANACHAMA
AFISA USHIRIKA JIJI LA MBEYA MAMA MASUBA AKISOMA AJENDA YA UCHAGUZI NA WAFUATAO WALIMAMA KUJINADI NA KUOMBA KURA ZAO MBEYA YA KADAMNASI
SONNY MWASELELA ( KUSHOTO), PETER MUSHI WAPILI (KUSHOTO), YUSTACK KALUMYANA WA PILI (KULIA) NA MWAKILISHI WA JOSHUA SALEHE NDG SHAIBU KAOSELA (KULIA)





WAWAKILISHI WAKIHESABU KURA
 AFISAH USHIRIKA AKITANGAZA WASHINDI
 WASHINDI WETU NI YUSTACK KALUMYANA (KUSHOTO) NA PETER MUSHI KULIA
 BAADA YA HAPO HATUA ILIYOFUATA NI KUFANYA UCHAGUZI KUMPATA MWENYEKITI WA CHAMA NA BODI NZIMA YA CHAMA
 HAWA NI BAADHI YA WAJUMBE WA BODI YA CHAMA WAKIJINADI KWA WANACHAMA
 MCHAKATO WA KUPATA MWENYEKITI WA CHAMA UNAENDELEA



 KURA ZIKIHESABIWA
 AFISA USHIRIKA ALIYEPEWA JUKUMU KUBWA LA KUSIMAMIA UCHAGUZI HUO AIKTANGAZA MATOKEO
 NA NDUGU ALLY MKAMI (KATIKATI) ALIIBUKA KIDEDEA KWA KUPATA KULA 516 NA HATIMAYE KUWA MWENYEKITI WA CHAMA
 BAADHI YA WANACHAMA WALIPITA MBELE NA KUMPONGEZA



MWENYEKITI WA CHAMA AKITOA SHUKRANI ZAKE ZA DHATI KWA UAMUZI WA

WANACHAMA KUMKABIDHI MAJUKUMU HAYO MAZITO YA KUKIONGOZA CHAMA

KUTOKA HAPA KILIPO NA KUENDELEA

NA BAADA YA HAPA ALIAHIRISHA MKUTANO MPAKA MWAKANI

WATAKAPOTANGAZIWA TENA

MENGI YALIZUNGUMZWA IKIWA NI PAMOJA NA UJEZI WA MRADI WA HOSTEL ZA

 CHAMA, KUFANYA SHUGHULI ZA CHAMA KUENDANA NA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

NA KUWAASA WANACHAMA KUNUNUA HISA KWA WINGI ILI KUWEKEZA NDANI YA

CHAMA HICHO ILI WAWEZE KUWA WAMILIKI HALALI WA CHAMA NA MALI ZAKE

PICHA ZOTE NA FREE MEDIA TO BLOGS

JE,UMEISIKIA HII POPOTE PALE AU UNATAKA KUISIKIA HAPA?

Makinda: Wabunge waliotemwa wamepigika

Adai wanakwenda ofisini kwake kuombaomba
 
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amesema kuwa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi inayowakabili wabunge wanapomaliza vipindi vyao, ofisi yake imelazimika kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili waweze kumudu maisha.
Makinda alitoa kauli hiyo jana wakati akibadilishana mawazo na Spika wa Bunge la Uswisi, Maya Graf ambaye yupo nchini kwa mapumziko mafupi na familia yake.
Alisema kuwa kwa kipindi alichokaa katika kiti cha uspika, amebaini matatizo ya kiuchumi yanayowakabili wabunge waliostaafu.
Makinda alisema kuwa wabunge wengi wamekuwa wakiathirika kiuchumi pindi wanapotoka katika nafasi hiyo, hivyo mafunzo yatawawezesha kuwa na shughuli za kufanya, na kwamba yatatolewa kwa wabunge wote.
Alisema kuwa ni muhimu wabunge wakaichukulia siasa kuwa sio kazi ya kudumu ili wanaposhindwa kuchaguliwa, wafanye shughuli nyingine za kuwaingizia kipato.
“Hata ukiangalia magomvi yanayotokea wakati wa uchaguzi, wengi wasiokubali matokeo ni wale ambao hawana shughuli za kufanya,” alisema.
Spika Makinda alisema kuwa kwa wabunge ambao wana shughuli za kufanya, kwao ubunge unakuwa sio tatizo kwa kuwa wana uwezo wa kuendesha maisha yao.
Alisema tangu ashike nafasi hiyo, wabunge wengi walioshindwa uchaguzi wamekuwa wakifika ofisini kwake na kuomba msaada wa kifedha wakati ofisi hiyo haina fungu la wastaafu hao.
“Kuna siku nilikuwa ofisini walikuja wabunge wastaafu zaidi ya watano wakiomba msaada, ikanilazimu nitoe akiba yangu nikawasaidia baadhi, lakini wale ambao hawakupata chochote walinung’unika sana,” alisema.
Makinda alisema kuwa kabla ya mwaka 1995, Bunge liliweka utaratibu wa pensheni kwa wabunge wastaafu, lakini uliondolewa na anachopata sasa mbunge ni posho ya kumaliza vipindi vyake vya ubunge.
Alisema kuwa na hiyo inatokana na mishahara midogo wanayopata wabunge ukilinganisha na mabunge mengine.
“Hata ukiangalia fedha unayopata, unatakiwa kuigawa na nyingine kupeleka jimboni, nyingine wengine wanatumia wakati wa uchaguzi jambo linalofanya mbunge akikosa kuchaguliwa akose la kufanya,” alisema.
Naye Graf, alisema kuwa wabunge wa nchi yao hawana shida pale wanaposhindwa kuchaguliwa kwa kuwa wana uwezo wa kupata kazi nyingine, na ajira sio tatizo.