Jumamosi, 21 Desemba 2013

KIKWETE AFUKUZA MAWAZIRI WANNE

 
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania amewafukuza kazi mawaziri wanne baada ya kutengua uteuzi wao kwa tuhuma za kushindwa kusimamia operesheni ya kuwasaka majangili.
Hatua hii ya Rais Kikwete ya kutengua uteuzi unatokana na shinikizo la Bunge la Tanzania ambao walitaka mawaziri hao wajiuzulu wenyewe au rais awafukuze kazi kutokana matukio ya mauaji, utesaji na uvunjifu wa haki za binadamu wakati wa operesheni hiyo uliofanywa na watendaji walio ndani ya wizara zao.
Mauaji, utesaji na ukiukaji wa haki za binadamu wakati operesheni ulifichuliwa na taarifa ya kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na utalii iliyopewa jukumu ya kufanya uchunguzi baada ya kuwepo kwa malalamiko kuwa operesheni hiyo uliambatana na ukiukaji wa haki za binadamu.
Miongoni mwa mateso na ukiukwaji wa haki za binadamu uliotajwa kwenye ripoti ya kamati hiyo ilikuwa ni mauaji, utesaji ikiwemo kuwalazimisha baadhi ya wanaume kufanya mapenzi na miti au wanyama waliokufa.