Alhamisi, 14 Novemba 2013

TANZANIA YAZIDI KUKAMATA MENO YA TEMBO

 
Meno ya Tembo

Kwa mara nyingine katika kipindi kisichozidi wiki mbili, polisi nchini Tanzania wamenasa shehena kubwa ya meno ya tembo yakiwa yamefichwa katika kontena, bandarini Zanzibar.
Watu wawili wamekamatwa wakihusishwa na meno hayo.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, meno hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika kontena la futi arobaini yakiwa yamechanganywa katika mifuko iliyohifadhi makombe ya konokono wa baharini, tayari kwa kusafirishwa nje.
Kamishna Mussa amesema, kwa sasa kiasi hicho cha meno ya tembo bado hakijafahamika kutokana na kuendelea kwa kazi ya kupakua kutoka kontena hilo.
Hivi karibuni raia watatu wa China walikamatwa nchini Tanzania kwa kukutwa na meno 706 ya tembo, sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi mbalimbali nchini humo.
Kukamatwa kwa meno haya ya tembo, kumekuja wakati tayari serikali imetangaza kusitisha Operesheni Tokomeza Ujangili, ambayo ililenga kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka kutokana na kuuawa katika hifadhi za taifa nchini Tanzania. Wanyama wanaolengwa zaidi na majangili kutokana na meno yao na pembe ni tembo na faru.
Matukio ya kukamatwa kwa meno ya tembo kutoka Afrika Mashariki yamekuwa yakiripotiwa kila mara. Oktoba, 20, 2012, tani nne za meno ya tembo yenye thamani ya dola milioni 3.4 za Kimarekani yalikamatwa Hong Kong, yakidaiwa kusafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.
Pia Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18 sawa na dola zaidi ya elfu 11, yakisafirishwa kwenda nje.
 

HII NI HATARI NA JAMII INAPASWA KUCHUKUA HATUA...! MBUNGE ADAIWA KUBAKA,KUMPA MIMBA NA KUMWAMBUKIZA VIRUSI MWANAFUNZI MWENYE UMRI WA MIAKA 16

 MBUNGE wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), ameingia katika matata. Katika kujaribu kudhibiti mtoto wa shule ambaye anadai alibakwa naye na kuambukiwa virusi vya ukimwi, mbunge huyo ametoa vitisho vya kuua mtoto huyo na kujiua kama njia ya kuepuka dhahama inayoelekea kumkabili. Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti habari za mbunge mmoja (bila kumtaja jina), jana asubuhi Profesa Kapuya ameibuka na kumtisha mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 anayesoma Shule ya Sekondari Turiani iliyoko Magomeni jijini Dar es Salaam.
Baada ya kujua kuwa mtoto huyo ndiye alitoa habari za masahibu hayo, ambayo mbunge hakutaka yajulikane, alimpigia simu mtoto huyo, na baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.
Jana Tanzania Daima ilishuhudia baadhi ya meseji za simu zilizotumwa na Profesa Kapuya kwenda kwa mtoto huyo.
Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993930, Profesa Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: “chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?”
Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.
“Mwambieni Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi. Si mmemuingizia hela leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote.
“Jana si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha, maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani anawakamata? Nani atapigana nasi?”
Hata hivyo, baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha alikuwa anafikiria kunywa sumu..
Ujumbe huo uliotumwa kwa mtoto huyo saa 11:2 3 ulisema: “nimwakosea sana, acha nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie mje mnizike.”
Hasira za Profesa Kapuya dhidi ya mtoto hao zilitokana na hatua ya mtoto huyo na dada yake kufichua unyama wanaodai kutendewa na mbunge huyo, ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.