Jumatano, 6 Novemba 2013

MATUKIO KATIKA PICHA

 
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH JAKAYA M.KIKWETE AKITOA HESHIMA ZAKE ZA MWISHO KWA MWILI WA ALIYEKUWA JAJI MSTAAFU HILARY MKATE JIJINI DAR ES SALAAM SIKU YA JUMA TATU
GARI LA SERIKALI LIKIWA IMEFUNIKWA NAMBA ZA USAJILI  MOJA YA GEREJI BINAFSI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM
MBUNGE WA SIMANJIO CHRISTOPHER OLE SENDEKA AKICHANGIA HOJA BUNGENI
MAREFA WAHITAJI ULINZI MKALI KUNUSURU MAISHA YAO WAWAPO KWENYE SHUGHULI ZA MICHEZO...PICHA HII NI REFA ALIYECHEZESHA MECHI YA LIGI KUU TANZANIA BARA YA SIMBA v KAGERA SUGAR
 

OFISI ZA CHAMA TAWALA NHINI CHINA ZAKUMBWA NA MILIPUKO YA MABOMU

 
Mabomu yaliyolipuliwa yalisemekana kuwa ya kutengenezwa nyumbani
Msururu wa milipuko midogo nje ya afisi za kimkoa za chama tawala cha Kikomunisti,imesababisha kifo cha mtu mmoja
Maafisa wa polisi katika eneo hilo wamesema kuwa milipuko hiyo ilisababishwa na mabomu madogo yaliyotengenewa nyumbani.
Mlipuko huo uliotokea muda wa asubuhi wenye shughuli nyingi, ulisababisha kuvunjika kwa madirisha na moshi mkubwa kufuka.
Ripoti zilizotolewa na shirika la habari la kiserikali zilisema kuwa mabomu madogo yalikuwa yamefichwa ndani ya maua kando ya barabara.
Milipuko hiyo ilitokea Kaskazini mwa China katika eneo la, Tai-yuan, mkoani, Shanxi,
Taarifa za vyombo vya habari nchini humo vinasema kuwa watu 8 wamejeruhiwa na magari mawili kuharibiwa.
Picha zilizowekwa kwa mitandao ya kijamii imeonyesha moshi ukifuka pamoja na magari ya wazima moto ikiwa katika eneo la shambulizi ambalo lilitokea mapema asubuhi ya leo.
Hakuna taarifa za kina kueleza kiini cha milipuko hiyo. Hata hivyo kumekuwa ma matukio ya mara kwa mara ya wananchi kufanya mashambulizi kama haya dhidi ya serikali hasa wale ambao hawahisi kuridhishwa na serikali hiyo.
Hali ya wasiwasi pia imetanda hasa baada ya tukio la wiki jana mjini Beijing ambalo mamafisa walisema kuwa lilikuwa njama ya shambulizi la kigaidi.

WAASI WA M23 SASA WASALIMU AMRI DRC

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/05/131105120527__70910163_70910162.jpg 
Shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) linasema kuwa angalau watu 800,000 wametoroka makwao kufuatia vita kati ya serikali na waasi wa M23. Kundi hilo lilianza harakati zake dhidi ya serikali mwezi Aprili mwaka 2012.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/05/131105120555__70912492_70912491.jpg 
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, inasema kuwa wanajeshi wake wamekomboa ngome mbili za mwisho za waasi wa M23, Tshangu na Runyoni mapema Jumanne.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/05/131105120637__70912806_70912805.jpg 
Waasi wa M23 walitoroka maeneo waliyokuwa wameyateka ya sehemu za milimani nchini DRC baada ya jeshi la serikali kukataa ombi la kusitisha vita ili kufanya mazungumzo na serikali na hata kuwaondoa kutoka katika maeneo waliyokuwa wameyadhibiti.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/05/131105120608__70912800_70912799.jpg 
Jeshi la Congo liliungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuwapiga waasi wa M23 Mashariki mwa DRC.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/05/131105120540__70910166_70910165.jpg 
Rutshuru ni moja ya maeneo yaliyokombolewa na jeshi la serikali ya DRC, tangu mwishoni mwa wiki  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/05/131105120652__70913737_70913736.jpg 
Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini ni maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini na yamekuwa kitovu cha mgogoro wa kisiasa ambao umekuwa ukitokota DRC kwa miaka mingi.  

ENDELEA KUWA NASI KWA MATUKIO ZAIDI