Jumapili, 8 Septemba 2013

Watoto wa Somalia wahimizwa kwenda shule

Watoto wa Somalia
  Wakuu wa Somalia wameanzisha kampeni ya kuwapeleka shule watoto milioni moja.

Kampeni hiyo iitwayo "nenda shule" imeanza mjini Mogadishu na katika miji ya Somaliland na Puntland, yaani Hargeisa na Garowe, kwa msaada wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef.
Baada ya vita vya miongo mwili, Unicef inasema asili-mia-40 tu ya watoto wanakwenda shule Somalia - kati ya viwango vya chini kabisa duniani.
Unicef inasema mradi huo utawapa robo ya watoto wasiokwenda shule fursa ya kusoma.
Mradi utagharimu dola 117 milioni.

Tokyo yasherehekea kutuzwa Olimpiki 2020

Watoto wanaoneshana habari za magazeti kuwa Tokyo imechaguliwa kuandaa 2020 Olympics

Tokyo imekuwa ikisherehekea kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya mwaka wa 2020.
Mji mkuu wa Japan uliishinda kwa urahisi miji ya Istanbul na Madrid.
Tangazo hilo lilotolewa na rais anayeondoka wa kamati ya kimataifa ya michezo ya Olympiki Jacques Rogge lilishangiliwa sana mjini Tokyo.
Tokyo ni mji wa tano ambao utakuwa umeandaa Olimpiki mara mbili.
Mwandishi wa BBC amesema kuwa mji huo ulijitembeza vyema katika siku ya mwisho ya kampeni lakini piya ulionekana kuwa thabiti kifedha na kiusalama
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, aliiambia kamati ya Olimpiki, IOC, kwamba matatizo ya miyonzi ya nuklia katika kinu cha nishati cha Fukushima hayataathiri michezo mjini

Madawa ya Kulevya:Tanzania yaingia katika kashfa nzito


 Meli ya Tanzania iliyobeba madawa ya kulevya yenye thamani ya Sh. Bilioni 123 yazua kizaazaa nchini Italia!
 
 
Msemajia kutoka Italia amesema: 'The ship was intercepted after intelligence was received that it was carrying drugs - but we never expected such a huge consignment and for the crew to set her on fire.

'The idea was no doubt to try and destroy the evidence so that we could have no case against them but their plan failed and the fire was put out and the drugs were found during the search.

'Nine people on board jumped into the sea but they couldn't get very far as they were several miles from shore and they had to be rescued by Italian customs officers.

'The fire is now under control and the ship is being taken to a port where it will be thoroughly searched again and the nine crew members will be questioned by prosecutors.'

Kerry atafuta kuungwa mkono

John Kerry akizungumza juu ya Syria akiwa Marekani
Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry, anakutana na mawaziri wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu mjini Paris, akiendelea na ziara yake Bara la Ulaya kutafuta kuungwa mkono kuhusu kuiingilia kati kijeshi nchini Syria.
Hapo awali akiwa pamoja na mwenzake wa Ufaransa, Laurent Fabius, katika mkutano na waandishi wa habari, Bwana Kerry alisema kuwa nchi zaidi zinaunga mkono hatua ya kijeshi dhidi ya Syria kwa kutumia silaha za kemikali mwezi uliopita.
Ufaransa inaiunga mkono Marekani kuhusu Syria, lakini kama wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya, inataka kusubiri ripoti ya wachunguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa waliozuru Syria.