Jumapili, 13 Julai 2014

LEO KATIKA MATUKIO YA PICHA

LIVE MUDA HUU: KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA KANISA LA TAG, UWANJA WA SOKOINE MBEYA. MGENI RASMI NI RAIS DK. JAKAYA KIKWETE.













Picha na Mbeya yetu Blog

Endelea kufuatilia hapa

HII NI ZAIDI YA UJUAVYO....UGONJWA WA EBOLA NI JANGA KWA AFRIKA HASA MAGHARIBI

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131439__75930220_msb8380_medium.jpg 
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka "hatua za dharura" zichukuliwe ili kudhibiti kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Africa magharibi, ambao umewauwa zaidi ya watu 400. Ugonjwa huu ndio mkubwa zaidi duniani kuzuka kutokana na visa vyake, vifo na kusambaa katika maeneo.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131441__75930223_msb8345_medium.jpg
Kumekuwepo na visa visivyopungua 600 nchini Guinea - ambapo ugonjwa huo ulianza kuzuka miezi minne iliyopita mjini Guekedou, ambao ulikuwa kituo kikubwa cha biashara, kilichowavutia wauzaji na wanunuzi kutoka mataifa kadhaa.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131446__75930386_msb8353_medium.jpg
Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres (MSF) tayari limeonya kuwa kusambaa kwa ebola hakuwezi kudhibitiwa. Shirika hilo lina wafanyikazi 300 wa kimataifa na vile vile wa kitaifa wanaofanya kazi nchini Guinea, Sierra Leone pamoja na Liberia, ambako ugonjwa huo unaenea kwa kasi. Mataifa mengine yako 
macho iwapo ugonjwa huo utasambaa Zaidi.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131523__75931214_msb8358_medium.jpg
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na ambao dalili zake za mwanzo huweza kuwa kushikwa na homa, kuwa dhaifu, kuumwa na misuli na kuumwa na koo. Na huo ni mwanzo tu: kile kinachofuata ni kutapika, kuendesha na -wakati mwingine- kuvuja damu.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131458__75930623_msb8400_medium.jpg
Virusi hivyo huenea kwa haraka sana, na hadi sasa hakuna dawa inayotambulika kuweza kuvitibu, kwa hivyo wanaotoa huduma za matibabu huvalia mavazi yanayowakinga kutokana na kuambukizwa kwa ugonjwa huo. Kulingana na uzito wa athari za ugonjwa huo, hadi kufikia asilimia 90 ya walioambukizwa huaga dunia. Anayehakikisha usafi anawakaribia wagonjwa wanaosubiri matokeo baada ya kupimwa damu.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131456__75930581_msb8385_medium.jpg
 Vipimo vya maabara vitaonyesha kwa saa kadhaa iwapo sampuli ya damu inayopimwa ina virusi vya Ebola au la.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131450__75930518_msb8378_medium.jpg
Baada ya kukumbana na virusi hivyo katika sehemu iliyotengwa, mavazi na viatu husafishwa kwa Chlorine.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131443__75930225_msb8344_medium.jpg
Kando na kutoa huduma za kliniki, kikundi hicho hutoa hamasisho kuhusu ugonjwa huo. Hapa Touloubengo, familia tano ambazo nyumba zao zilikuwa zimesafishwa siku kadhaa zilizopita kutokana na kuaga dunia kwa mmoja wao wanakabidhiwa magodoro.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131448__75930451_msb8366_medium.jpg
Sio kila mtu aliye salama. Hapa familia ya Kinda Marie Kamano, akiwemo dadake (katikati), pamoja na wanajamii wengine wanahuzunika katika mazishi yake karibu na nyumba yake.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131453__75930538_msb8381_medium.jpg 

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131500__75930666_msb8383_medium.jpg 
Takriban watu 600 wamefariki kutokana na homa ya Ebola Afrika Magharibi


Endelea kufuatilia