Mbita ni moja wapo wa miji inayozingira Ziwa Victoria.
Timu ya Sema Kenya ilifika huko kuhamasisha wenyeji kujiunga na mijadala ya utawala katika kipindi kila wiki.
Msafara huu uliwafikia wengi.
Wakazi mbalimbali walijitokeza kusikiliza habari.
Walipata nafasi ya kujadili masuala tofauti inayowahusu kama wakazi wa Mbita.
Wakazi wa Mbita walipata burudani na habari kutoka timu ya Sema Kenya walipozuru mji huo katika msafara.