Bingwa wa mchezo wa Kung fu
nchini Misri, Mohammed Youssef amevuliwa medali yake ya dhahabu baada ya
kuonesha ishara ya kumuunga mkono Rais wa Misri aliyeondolewa
madarakani, Mohamed Morsi.
Serikali ya Misri imekuwa ikipambana na waandamanaji tangu baada ya Morsi kuondolewa madarakani mwezi Julai.
Kaka wa mwanamichezo huyo Hammam amesema Youssef alirudishwa nyumbani kutoka kwenye mashindano hayo na kuhojiwa alipowasili nchini mwake.
Mkurugenzi wa chama cha Kung Fu nchini Misri, Gamal El-Jazzar amesema Youssef atafungiwa kuiwakilisha Misti kwenye michuano ya dunia ya mchezo huo, hata hivyo haijafahamika kama atafungiwa moja kwa moja.