Ijumaa, 20 Septemba 2013

Polisi wakosoa uchunguzi wa Marikana



Wafanyakazi wa Marikana waligoma wakidai nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi

Polisi nchini Afrika Kusini wameikosoa tume inayochunguza mauaji ya wafanyakazi thelathini na nne katika mgodi wa madini ya platinum huko Marikana Agosti mwaka uliopita kusema kuwa walidangaya.
Katika taarifa idara ya polisi imesema kuwa madai dhidi yao ni ya kuudhi na hayana msingi.
Wamesisitiza kuwa walitumia risasi kujilinda walipokuwa wakijaribu kuwatawanya na kuwapokonya silaha wafanyikazi hao waliokuwa wakigoma.

87 wauawa na Boko Haram Nigeria



Mashambulizi yameongezeka tangu jeshi la Nigeria kuanza vita dhidi ya Boko Haram

Wapiganaji wa Boko Haram wamewaua watu 87 katika shambulio katika Jimbo la Borno nchini Nigeria.
Mashahidi wanasema kuwa wapiganaji hao waliteketeza nyumba kadhaa katika tukio hilo la kutisha mnamo Jumanne usiku.
Shambulio hili limetokea siku chache baada ya makabiliano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Boko Haram

Hakimu achomwa kisu mahakamani


Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga wakimuhudumia hakimu Satto Nyangoha aliyechomwa kisu shavuni jana, akiwa mahakamani na mlalamikaji katika kesi ya wizi wa baiskeli, Emmanuel Izengo

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.
Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo,