Ijumaa, 20 Septemba 2013

Polisi wakosoa uchunguzi wa Marikana



Wafanyakazi wa Marikana waligoma wakidai nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi

Polisi nchini Afrika Kusini wameikosoa tume inayochunguza mauaji ya wafanyakazi thelathini na nne katika mgodi wa madini ya platinum huko Marikana Agosti mwaka uliopita kusema kuwa walidangaya.
Katika taarifa idara ya polisi imesema kuwa madai dhidi yao ni ya kuudhi na hayana msingi.
Wamesisitiza kuwa walitumia risasi kujilinda walipokuwa wakijaribu kuwatawanya na kuwapokonya silaha wafanyikazi hao waliokuwa wakigoma.

Mawakili katika tume hiyo ya Marikana wamelaumu polisi kwa kutoa ushahidi wa uongo kuhusu hatua ya kutumia risasi wakitaka ukubalike bila upinzani.
Baada ya kuchunguza kwenye Kompyuta za polisi walisema kuwa polisi walikuwa wamezuilia na kubadilisha yaliyokuwemo katika stakabadhi hizo.
Tume hiyo kwa mara nyingine imeakhirisha vikao vyake inapopitia maelfu ya stakabadhi zinazohusiana na tukio hilo.
Sasa polisi wanasema kuwa wamekuwa wakishirikiana na tume hiyo ya Marikana kikamilifu bila vikwazo vyovyote. Kadhalika wanataka wapewe nafasi kujieleza kabla ya mawakili kutoa hukumu.


Hakuna maoni: