Jumanne, 8 Oktoba 2013

TAZARA FC YAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA TSHS 300,000/= TOKA CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO TAZARA MBEYA WORKSHOP(MBESACCO)

MWENYEKITI WA CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO CHA TAZARA MBEYA WORKSHOP (MBESACCO) NDG JACOB MBOGO (KULIA) AKIKABIDHI JEZI KWA AFISA MWAJIRI WA SHIRIKA LA RELI LA TANZANIA NA ZAMBIA (TAZARA) NDG MCHABA MGWENO (KUSHOTO) -MBEYA

NAHODHA WA TIMU YA TAZARA FC NDG BETHUEL KAGIMBO (KUSHOTO) AKITOA MKONO WA PONGEZI KWA MWENYEKITI WA CHAMA NDG JACOB MBOGO (KULIA)
 
NAHODHA MSAIDIZI WA TAZARA FC NDG HANSI AMANYISYE (KUSOTO) NAE AKITOA PONGEZI ZAKE KWA MWENYEKITI WA CHAMA HICHO CHA MBESACCO.
 OFISI ZA CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO CHA TAZARA MBEYA WORKSHOP..NI MAZUNGUMZO NA SHUKURANI BAADA YA MAKABIDHIANO YA VIFAA HIVYO VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA TSHS 300,000/=
HII NI PICHA YA PAMOJA MARA TU BAADA YA MAKABIDHIANO HAYO KUFANYIKA..NA HIZO NI BAADHI YA JEZI ZILIZOKABIDHIWA KWA TIMU HIYO INAYOJIANDAA KUSHIRIKI LIGI DARAJA LA NNE MWAKA HUU
AFISA MWAJIRI WA TAZARA-MBEYA NDG. MCHABA MGWENO (KATIKATI KUTOKA KULIA) AKIONGEA NA MANAHODHA WA TIMU AKIWATAKA KUTUMIA VYEMA FULSA HIYO YA MICHEZO NA KUJITUMA KWA NGUVU ZOTE NA KULETA MAFANIKIO KATIKA TIMU YAO

PAMOJA NA MSAADA HUO KUKABIDHIWA KWA TIMU HIYO BADO CHANGAMOTO NI NYINGI KWAO KWANI WANAHITAJI VIFAA VINGI ZAIDI IWEZEKANAVYO IKIWA PAMOJA NA MCHANGO WA KIINGILIO KWA AJILI YA LIGI WENYE THAMANI YA TSHS 120,000/= PAMOJA NA  MIPIRA TIMU IWAPO KWENYE MAZOEZI YA KILA SIKU.

PICHA NA free media to blogs

DUNIA INATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA AL SHABAAB





Wanamgambo wa al-Shabab wamedhibiti hali katika mji wa Barawe, ambako makomando wa Marekani walijaribu kumkamata mmoja wa viongozi wa kundi hilo mnamo Jumamosi.

Wenyeji wa mji huo wameambia BBC kuwa takriban makomando 200 waliojifunika nyuso zao wamewasili mjini humo wakiwa na silaha nzito.

HII SIYO TANZANIA TU..:MAANDAMANO YA WALIMU BRAZIL YAZUA GHASIA


Walimu wamekuwa wakidai mishahara bora kwa muda mrefu

Maandamano ya watu waliokuwa wanaunga mkono walimu wanaodai mishahara bora zaidi nchini Brazil, yamegeuka na kuwa makabiliano kati yao na polisi katika miji ya Rio de Janeiro na Sao Paulo.

Mji wa Rio ulikuwa umesongamana watu zaidi ya 10,000 wakiandamana kwa amani .
Lakini usiku ulipoingia, waandamanaji kadhaa walirusha mabomu ya moto katika majengo ya serikali nao polisi wakawarushia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya.

Maandamano sawa na hayo yalitokea mjini Sao Paulo na pia kusababisha ghasia na makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji hao waliokuwa wamefunika nyuso zao na kuvamia benki.
Hali ya usalama nchini Brazil, ni changamoto kubwa ambayo huenda ikajitokeza zaidi wakati wa kombe la dunia mwaka 2014 na michezo ya olimpiki mwaka 2016 .

Maandamano ya hivi karibuni yalidumu kwa masaa kadhaa na yalikuwa salama mwanzoni.
Lakini usiku ulipoingia ghasia zikazuka huku waamdanamanaji wakiteketeza majengo ya serikali na wengine kuvamia benki na kuvunja mashine za pesa. Baadhi ya benki ziliteketezwa.

Waandamanaji hao pia waliiba viti kwenye benki na kuvitumia kama vizuizi kati yao na polisi.
Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozu kurejesha utulivu.Walimu wamekuwa wakidai nyongeza ya mishahara kwa miezi kadhaa sasa. 

Takriban watu 50,000 walikadiriwa kuandamana ili kuwaunga mkono walimu kabla ya ghasia kuzuka lakini polisi waliweza tu kuthibitisha watu 10,000 walishiriki maandamano hayo.

LAMPEDUSA: WATU 232 IKIWA NI IDADI RASMI YA WALIOFARIKI



Wanajeshi wakisaidia na juhudi za kuokoa maiti

Wapiga mbizi nchini Utaliana wamapeta idadi kubwa ya maiti katika boti iliyozama na ambayo ilikua imewabeba wahamiaji wa kiafrika kwenda Ulaya siku ya Alhamisi.

Miili 38 iliweza kuondolewa kwenye boti hiyo ambayo wapiga mbizi walikuwa na changamoto kubwa kuweza kuifikia. Idadi rasmi ya waliofariki imesemekana kuwa watu 232.

Wapiga mbizi waliweza kupata watu waliokuwa wamekwama sehemu moja ya boti hiyo kwa mujibu wa maafisa wa huduma za meli akiongeza kuwa ilikuwa imekwama pamoja na kuwapa wakati mgumu kuiondoa miili hiyo.

Boti hiyo ilishika moto na kisha kuzama karibu na kisiwa cha Lampedusa eneo la Sicily.
Manusura wa ajali hiyo iliyotokea umbali wa kilomita moja kutoka ufuoni walikuwa 155.
Juhudi za kuokoa miili kutoka katika boti hiyo zilisitishwa wakatai za usiku lakini zitaanza tena Jumanne

Maelfu ya wahamiaji wa kiafrika hujaraibu kufanya safari hatari za majini kutoka Afrika ya Kaskazini hadi katika kisiwa cha Sicily na katika visiwa vingine nchini Utaliana na ajali hutokea mara kwa mara lakini hii ya wiki jana ilikuwa moja ya ajali mbaya zaidi kuwahi kutokea katika safari za wahamiaji kwenda Ulaya.

Mabaki ya meli hiyo yako mita 47 chini ya bahari maana kuwa wapiga mbizi wanaweza kukaa chini ya bahari kwa muda mfupi tu.

Idadi kubwa ya miili imeweza kutolewa kwenye boti hiyo lakini inaaminika kuna miili mingine zaidi ambayo imekwama ndani ya boti.

IKULU: JK HAJASAINI MUSWADA WA KATIBA

IKULU imekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii jana ikidai kuwa Rais Jakaya Kikwete ametia saini muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba ambao ulipitishwa na Bunge.

Taarifa iliyotolewa jana jioni na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza mambo manne kufafanua hatua za muswada huo kusainiwa na Rais Kikwete utakapomfikia.
Ilisema kuwa Ofisi ya Rais, Ikulu, haijapokea muswada huo kwamba inawezekana umekwishakutumwa kutoka bungeni lakini haujamfikia Rais, hivyo kama haujamfikia hawezi akawa ameutia saini.

“Pili, muswada huo ukimfikia inatarajiwa kuwa atautia saini kwa sababu umepitia katika mchakato sahihi na halali wa kikatiba kwa maana ya kufikishwa bungeni na serikali, kujadiliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge.
“Tatu, kama yapo marekebisho ambayo yanaonekana yanafaa kufanywa katika sheria hiyo, basi yatafanywa na Bunge baada ya Rais kuwa ametimiza matakwa ya kikatiba ya kutia saini muswada ambao umepitishwa na Bunge,” ilisema taarifa hiyo.

Katika sababu ya nne Ikulu ilisema kuwa hii haitakuwa mara ya kwanza kwa sheria kupitishwa na Bunge, ikatiwa saini na Rais na baadaye kufanyiwa marekebisho na Bunge baada ya kuonekana umuhimu wa kufanya marekebisho hayo.

Katika hatua nyingine, Ikulu imeanza mawasiliano na viongozi wa vyama vya siasa nchini vyenye hoja kuhusu muswada huo kwa nia ya kuandaa mkutano kati yao na Rais Kikwete.
Taarifa ilisema kuwa mawasiliano hayo yalianza jana kufuatia maelekezo ya Rais Kikwete kwa Ofisi ya Katibu wa Rais.

Kufuatia matukio yaliyotokea bungeni wakati wa kujadiliwa na kupitishwa kwa muswada huo na kauli mbalimbali za wabunge wa vyama vya upinzani na wadau wengine, Rais Kikwete alisema kuwa hoja na kauli za wanaopinga muswada huo zinazungumzika kwa nia njema ya kutafuta mwafaka katika mchakato wa kutafuta Katiba mpya.

“Kwa mujibu wa maandalizi hayo, Ofisi ya Rais, Ikulu, inaangalia uwezekano wa kuitisha mkutano huo Jumapili ya Oktoba 13 au Jumanne ya Oktoba 15, mwaka huu,” ilisema taarifa hiyo.
Hofu ya wengi

Kufuatia kuzagaa kwa taarifa hiyo, matumaini ya wengi yaliyeyuka baada ya ratiba ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kutoonyesha jambo hilo kama linarudi bungeni.
Wadau wengi walitumaini kuwa Rais Jakaya Kikwete asingeusaini muswada huo, kufuatia kauli yake ya kuwataka viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi waachane na maandamano ya kuupinga na badala yake waketi na kujadiliana na serikali.

Akizungumza juzi na waandishi wa habari, Lissu ambaye ni mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, alisema kuwa busara ya Rais kutaka mjadala na wapinzani ingeonekana jana kwenye ratiba ya kamati.

Alisema kama Rais hajausaini muswada huo, ratiba ya Kamati ya Bunge ilipaswa kuonyesha kuwa sasa unarudishwa bungeni kufanyiwa marekebisho ya kasoro zinazolalamikiwa.

Hata hivyo, jana ratiba hiyo iliyotolewa kwa wajumbe wa kamati hiyo, haikuonyesha jambo lolote kuhusu muswada huo unaopigiwa kelele, jambo lililozua hisia kuwa umeishatiwa saini na Rais.
Lissu alisema licha ya Rais Kikwete kusema jambo hilo linazungumzika, sasa amemaanisha kuwa hana nia ya kutosaini muswada huo wenye mapungufu mengi.

Katika ratiba ya kamati ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kupata nakala yake, wajumbe wake sasa wamepangiwa ratiba ya siku tatu kuanzia Oktoba 9 hadi 12 kwenda Zanzibar kukusanya maoni ya wadau kuhusu miswada ya sheria ya kura za maoni 2013 na sheria ya mbadiliko ya sheria mbalimbali ya mwaka 2013.

Mbowe afunguka
Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe, amesema kuwa Kikwete amemkosea Tundu Lissu kwa kumuita mwongo, mzushi, mfitini na mzandiki na kwamba anapaswa kumwomba radhi.

Akifungua semina ya siku tatu ya mafunzo ya wakufunzi wa kanda za CHADEMA jana jijini Dar es Salaam, Mbowe alimtahadharisha Rais Kikwete kuwa makini na suala la Katiba kwani ni roho ya nchi.

Alisema Katiba ni sheria mama na suala linaloweza kulete mpasuko, hivyo anapolizungumzia awe amejiridhisha kuliko kutegemea maneno ya kuambiwa, kufahamishwa, kuelezwa na washauri wake ambao wamekuwa wakimshauri vibaya na wakati mwingine kumdanganya.
“Rais awe makini na kauli zake kabla ya kuzungumza na Watanzania na atumie fursa hiyo kujiridhisha na katika suala la Katiba asifanye utani,” alisema.

Alisema kuwa katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, Rais Kikwete ametangaza uhasama binafsi na Lissu kutokana na hotuba aliyotoa bungeni.
Mbowe alisema Rais amemwonea Lissu na kwamba hata mkubwa akikosea huomba radhi, hivyo katika hilo anapaswa amwombe Lissu radhi.

“Lissu alikuwa akitimiza wajibu wa kibunge, alifanya hayo kwa mujibu wa kanuni za Bunge na alikuwa anawakilisha maoni ya kambi ya upinzani.
“Nashindwa kuelewa kwa nini Rais hakuelewa hili na maneno aliyotumia sio maneno ambayo Rais anapaswa kuyatumia anapohutubia wananchi,” alisema.

Aliongeza kuwa inashangaza kuona Rais Kikwete hana utamaduni wa kujisomea, kwamba asingesema mjadala wa bungeni ulienda vizuri bila kusoma kumbukumbu za Bunge (Hansard) au kuangalia mikanda iliyorekodiwa.
“Amezingatia ushauri wa mawaziri wake, kukubali hata mambo ambayo yamechomekwa katika muswada ulioletwa bungeni,” alisema Mbowe.

Mapema akifungua semina hiyo, alisema CHADEMA imetambua vipaji mbalimbali katika ngazi za uongozi, hivyo imegatua madaraka kupeleka kwenye kanda badala ya mamlaka yote kutolewa na makao makuu.

Aliongeza kwamba mkakati uliopo sasa wa CHADEMA ni kuifanya kuwa ya kidijitali (cha kisasa) katika maana kuwa wakufunzi wapya wataendesha chama kitaalamu.

Wadau wanena
Wadau mbalimbali wamepokea kwa mitazamo tofauti hotuba ya mwisho wa mwezi ya Rais Kikwete ambayo imeonyesha mgawanyiko juu ya mchakato wa Katiba unapoelekea.
Wakizungumza na Tanzania Daima jana kwa nyakati tofauti, wadau hao walisema kuwa tangu kuanza kwa mchakato huo umekuwa na dosari, hatua inayoashiria kuwa kuna uwezekano wa kushindwa kuafikiana.

Mhadhiri wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, alisema kuwa ni wazi kuwa mchakato huo unaashiria kushindwa kupatikana kwa muafaka.
Alisema kuwa mchakato huo umevamiwa na wanasiasa na wameuathiri hivyo itakuwa ndoto kupata Katiba iliyo ya Watanzania.

“Mjadala huu umeingia dosari tangu mwanzo kuanzia kutungwa kwa sheria yenyewe na hata kuundwa kwa tume ambayo ina sura za mgawanyiko kwani wale waliopo kila mmoja ana maslai yake binafsi na sio tume ya kitaifa,” alisema.

Mhadhiri huyo alisema kuwa Katiba inatungwa kwa kuketi chini na kujadiliana na sio kama inavyotokea ambapo wanasiasa wamebadili muelekeo na kuitana majina ya wanafiki na wazandiki, jambo ambalo linaashiria kutokuamiana.

Naye mhadhiri mstaafu wa chuo hicho, Dk. Azavel Lwaitama, alisema kuwa lugha aliyotumia Rais Kikwete inaonyesha kuwa ni wa kundi la Chama cha Mapinduzi (CCM).
Alisema kuwa Rais ameonyesha nia ya kutaka kusaini muswada huo na hilo linaashiria kuwa Katiba itakayopatikana itakuwa ni ya CCM.

“Kama Rais Kikwete kaonyesha nia ya kutaka mchakato uendelee na asaini huo mswada basi hakuna haja ya kukutana na wapinzani kama anavyotaka; itakuwa ni sawa na kupoteza muda tu na wala haja ya kurudisha bungeni,” alisema.

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Habari na Haki za Binadamu wa CUF Zanzibar, Salum Bimani, alisema kuwa kama hotuba ya Rais Kikwete itaweza kutekelezwa kuna uwezekano wa kupatikana kwa Katiba ya Watanzania

CHANZO>>>>MTANZANIA