Kwa siku mbili zijazo, Wamisri watajua ikiwa watakuwa na katiba mpya au
ikiwa rasimu ya katiba inayopigiwa kura haitaidhinishwa.
Nchi hii imekuwa ikikumbwa na hali ngumu ya kisiasa tangu mapinduzi ya kiraia yaliyomwondoa mamlakani Hosni Mubarak.
Baadhi walihisi huo ndio ulikuwa mwisho wa siasa mbaya lakini baadaye
rais aliyechaguliwa kihalali Mohammed Morsi, aliondolewa mamlakani na
jeshi
Morsi alikuwa mwanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo ikiwa
katiba hii itapitishwa ndio itakuwa mwisho wake. Chini ya Katiba mpya
Vyama haviwezi kuundwa kwa misingi ya kidini, kabila, jinsia na
kijiografia. Bila shaka itakuwa pigo kubwa kwa vuguvugu la Muslim
Brotherhood
Misri pia imekuwa ikikumbwa na hali mbaya ya usalama. Mashambulizi ya
kulipiza kisasi na ya kuvizia yakiwa jambo la kawaida. Chini ya katiba
hii waziri wa ulinzi sharti awe mwanajeshi kama hali ilivyo sasa.
Usalama ulidhibitiwa kote nchini humo kwa hofu ya mashambulizi
Wake kwa waume, wazee kwa vijana wote walijitokeza kwa hamu ya kuipatia Misri mustakabali mwema wa kisiasa