Raia wa Ufilipino wangali wanahisi athari za Kimbunga Haiyan,
kinachojulikana na wenyeji kama Yolanda. Kimbunga hicho kilifanya
uharibifu mkubwa sana baada ya kupiga eneo la Kati mwa Ufilipino Ijumaa
na Jumamosi. Inahofiwa maelfu ya watu wamefariki kutokana na Kimbunga
hicho.
Picha zaidi zilizopigwa kutoka angani, katika mji wa Tacloban moja ya
maeneo yaliyoathriwa zaidi -lakini waokozi wangali kufika katika baadhi
ya maeneo yaliyoathirika ambako inahofiwa uharibifu mkubwa zaidi
ulifanyika.
Siku tatu baada ya Kimbunga hicho kinachosemekana kuwa kibaya zaidi
kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo , waathiriwa wako katika hali
mbaya.
Wakaazi wengi walijaribu kujiokoa lakini wakajipata katika vituo vya
kuwanusuru watu ambavyo navyo vilishindwa kuhimili mawimbi ya kimbunga
hicho.
Kuna afueni kwa wachache waliofika katika mkoa huu wa Lloilo, huku helikopta zikiwasili na msaada zaidi
Hapa katika mji wa Guiuan , mkoa wa Samar, wakaazi wanajisaidia kadri ya
uwezo wao , wakichukua chakula na hata kufanya msako katika moja ya
majumba yaliyosalia kusimama baada ya kimbunga
Nchi kadhaa zimeahidi kutoa msaada zaidi, lakini huku barabara zikiwa
zimezibwa na viwanja vya ndege kuharibiwa, tatizo litakuwa msaada huo
kuwafikia watu wanaouhitaji zaidi