Jumamosi, 31 Agosti 2013

TAZARA yagawanyika

Hapa ni Stesheni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia Mbeya
Hawa ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Stesheni mbalimbali wakiwa kwenye mshikamano kushinikiza uongozi wa shirika hilo kuwapa mishahara yao ya miezi minne sasa
Kwa nyuso za huzuni kabisa wanyakazi wa shirika la reli ya Tanzania na Zambia-Mbeya
Kushoto kwako ni mimi Alex Mwalyego nikijaribu kupata habari kadhaa kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo
Hapa wafanyakazi wakiondoka kwa huzuni bila kupata jibu lolote nini hatima ya mishahara yao

IGP Mwema ameibiwa upanga wa dhahabu wa kilo tatu




Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).

Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.

Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.

Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.

IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya kimataifa.

Upanga huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi katika nchi husika.

Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa kimataifa.

Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa Namibia.

Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Windhoek.

Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.

Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo.

Kichwa cha binadamu chapatikana katika ofisi ya mkuu wa polisi

Polisi nchini Kenya
Polisi nchini Kenya wanachunguza kisa ambacho kichwa cha mtu aliyeuawa kilipatikana kimewekwa nje ya afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya polisi Johnston Kavuludi jijini Nairobi.
Kifurushi hichi kilichokuwa kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile kilikuwa na mikono miwli ya binadamy iliyojaa damu.
kando ya kifurishi hicho kulikuwa na ilaani iliyoandiskwa ''Kavuludi wewe ndiye utakayefuata''.
Tangu uteuzi wake, kamishna huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia marekebisho idara ya polisi ambayo inadaiwa kuwa fisadi zaidi Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa idara ya polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na tukio hilo na kuwa bado wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.
Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo inayoongozwa na Kavuludi na ofisi ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana kuhusu nani ana madaraka ya kuliendesha idara hiyo.

Chanzo na BBC Swahili

Chelsea yashindwa kutamba mbele ya Bayern URFA Super CUP



Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye mechi ya jana...Ndani ya Dak 90 timu hizo zilikuwa (2-2)

Wachezaji wa Bayern wakifurahia ushindi wao baada ya kuiondosha Chelsea kwa Penalty (5-4) baada ya Rumelo Lukaku kukosa Penalty ya mwisho