Jumatatu, 1 Juni 2015

NDOA ZA JINSIA MOJA ZAPATA KIBARI...SHERIA MPYA YAANZISHWA

Kinara mkuu wa chama cha upinzani cha Labour nchini Australia, ameanzisha sheria inayokubalia ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, sheria ambayo inapingwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo, Tony Abbott.
Kiongozi huyo, Bill Shorten, amemtaka Bwana Abbott kuwakubalia wanachama wa serikali wawe na uhuru wa kupiga kura kuhusiana na swala hilo.
Abbot ambaye ni mfuasi wa kanisa katoliki alikataa kura ya uhuru wa ndoa za jinsia moja na kusema kuwa lengo lake kuu ni kuimarisha uchumi na usalama wa taifa.
***chanzo na BBC Swahili***

KAZI YA KUTANGAZA NIA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) BADO INAENDELEA...NI ZAMU YA MWANDOSYA MBEYA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kutangaza nia ya kugombea urais leo Juni Mosi na kuchukua fomu Juni tatu mwaka huu
.