Jumatano, 11 Desemba 2013

UHABA WA MABASI STENDI YA UBUNGO UNATISHIA MAISHA YA WASAFIRI

HAWA NI BAADHI YA WASAFIRI WAKIWA HAWAELEWI NINI HATIMA YA SAFARI YAO HII LEO

TAZAMA YANAYOENDELEA AFRIKA KUSINI

 
Mwili wa Mandela ukisindikizwa na polisi Afrika Kusini
Mwili wa hayati Nelson Mandela umewekwa katika jengo la Union ambako aliapishwa wakati aliingia mamlakani mwaka 1994.
Jeneza lake likiwa limefunikwa bendera ya taifa , lilipitishwa kwa umma likisindikizwa na msafara wa magari na pikipiki.
Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya union eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Mwili huo sasa utaweza kutizamwana wageni mashuhuri pamoja na wananchi wa kawaida.
Wageni hata hivyo hawaruhusiwa kupiga picha.
Mwili wa Mandela utawekw akatika hali hiyo kwa siku tatu zijazo hadi atakapozikwa Jumapili.
Leo jioni wasanii mbali mbali wa Afrika Kusini watashiriki katika tamasha maalum la kumuenzi Mandela na ambalo wananchji wataruhusiwa kuhudhuria bila malipo.