Ijumaa, 30 Agosti 2013

Maandamano kufanyika Misri licha ya kitisho cha serikali

Matukio ya Kisiasa

Maandamano kufanyika Misri licha ya kitisho cha serikali

Chama cha Udugu wa Kiislamu kimepanga kuandamana baada ya sala ya Ijumaa dhidi ya serikali ya mpito nchini humo. Maandamano hayo yameitishwa licha ya serikali kutishia kutumia nguvu kupambana na waandamanaji.
Maandamano haya ya leo yanatarajiwa kupima ni kwa kiwango gani vikosi vya usalama vimelidhoofisha kundi hilo na hii itajulikana tu kwa namna watu watakavyojitokeza katika maandamano hayo.
Kulingana na wakaazi huko, maandamano ya leo yanahofiwa kuzua machafuko zaidi katika nchi hiyo iliyokumbwa na msukosuko wa kisiasa.
Maandamano Misri Maandamano Misri
Umwagikaji mkubwa wa damu ulishuhudiwa wiki mbili zilizopita baada ya polisi kushambulia kambi za waandamanaji waliokuwa wanapinga hatua iliyochukuliwa Julai 3 ya kumuondoa madarakani kiongozi wao Mohammed Mursi kwa njia ya mapindzi ya kijeshi.
Hali hiyo ilisababisha vurugu ya wiki nzima zilizowauwa watu takriban 1,000, wengi wao wakiwa wafuasi wa Mursi. Inadaiwa kuwa baadhi ya wafuasi hao walijibu mashambulizi kwa kuchoma makanisa, majengo ya serikali na pia kushambulia vituo vya polisi.
Pande zote mbili zaombwa kusuluhisha tofauti zao
Katika mahojiano na shirika la habari la Associated Press, kiongozi wa kundi lililokuwa la waasi la Gamaa Islamiya, Abboud el-Zommor, alizihimiza pande zote mbili serikali na upinzani kukaa pamoja na kutatua tofauti zao ili kusimamisha umwagikaji wa damu nchini humo.
Huku hayo yakiarifiwa serikali imeongeza majeshi yake katika maeneo tofauti nchini humo huku ikilishutumu kundi la Udugu wa Kiislamu kuitisha maandamano na kuzua ghasia.
Kiongozi wa Udugu wa Kiislamu Mohamed El-Beltagi Kiongozi wa Udugu wa Kiislamu Mohamed El-Beltagi
Wakati huo huo utawala wa Misri umeendelea kuwakamata viongozi wa kundi hilo kwa madai ya kuchochea ghasia. Tayari viongozi wawili, Mohammed el-Beltagy na Khaled el-Azhari, walikamatwa hapo jana.
Polisi wanasema waliwakamata kwa sababu ya kuchochea maandamano na kuteswa kwa polisi aliyekamatwa na waandamanaji mjini Cairo.
Kwa upande wake. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imesema itapambana vikali na watu ambao wanajaribu kuyumbisha usalama wa nchi na kwamba polisi wamepewa amri ya kutumia nguvu katika kulinda mali ya umma na ile ya watu binafsi nchini humo.
Wizara hiyo imesema pia kuwa maandamano ya leo yana lengo la kusababisha vurugu.
Mwandishi: Amina Abubakar/Reuters/AP
Mhariri: Mohammed Khelef

DIAMOND AFANYA MAKUBWA KATIKA UZINDUZI WA VIDEO YAKE, AMKABIDHI GARI MUHIDIN GURUMO

1 1Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari aina ya Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki, Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini ikigharimu kiasi cha dola elfu 30.000 zaidi ya milioni arobaini za Tanzania, Video hiyo imetengenezwa kwa viwango vya kimataifa na itaweza kumtangaza vyema kijana huyo wa kitanzania katika ulimwengu wa muziki hasa kimataifa, Hafla hiyo imefanyika kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam na imehudhuriwa na wasanii pamoja na waigizaji wa filamu na watu maarufu mbalimbali
Mzee  Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo 3Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari 5Diamond akimuonyesha Mzee Gurumo gari 6Akimuelekeza jambo baada ya mzee Gurumo kuingia kwenye gari 7 
Diamond akizungumza machache kushukuru mashabiki wake na watu mbalimbali waliomsaidia kufikia hapo alipo



Diamond na madansa wake wakitumbuiza katika hafla hiyo 10Wasanii mbalimbali pamoja na MaDJ walikuwepo katika hafla hiyo hapa ni Dully Sykes na MawanaFA wakiwa na baadhi ya MaDJ 11Maurice Njowoka kutoka Cocacola wa pili kutoka kushoto na Mwanamuziki AY wa tatu kutoka kushoto pamoja na wadau wengine wakiwa katika hafla hiyo 12 
Mwigizaji Jaquiline Wolper naye alitia timu  13Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiwa na mama yake Diamond 15Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo 16 17Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari 18Hawa marafiki zangu wakakumbushia miaka kadhaa waliyofunga ndoa kwa kulishana mishikaki ilipendeza katikati ni Nancy Sumari akishuhudia 19Kulia ni Irene Uwoya kushoto Salma Msangi  20Kushoto AY na Salama Jabir wakipiga story na wadau mbalimbali 21 22Kutoka kulia ni Raymond Kigosi, Irene Uwoya na JB wakiwa katika hafla hiyo.
9

Zitto Kabwe: Msiwaamini wanasiasa, chama tawala wala wapinzani

Photo: Zitto Kabwe: Watanzania, msiwaamini sana wanasiasa; wawe wa chama tawala au wapinzani (Kuhusu uwajibikaji)

Soma zaidi hapa => http://bit.ly/12S5U8A Kauli hii ameitoa leo katika kongamano la ufuatiliaji wa uwajibikaji Jamii ambapo yeye alikuwa akiongelea majukumu ya bunge katika kusimamia uwajibikaji. Mambo mengi aliyoongea yalikuwa ni yenye mwelekeo chanya isipokuwa hili la kutupa tahadhari ya kutowaamini wanasiasa, akisisitiza hata wa upinzani. Nyuma ya kauli hii kumejificha nadharia nyingi kutegemea na mtu atakavyoipokea. Kwa maana nyingine, kauli hii inaleta hisia kwamba, hata wale wa chama chake tusiwaamini pia. Kwa kuwa mheshimiwa ni miongoni mwa members hapa, najua ujumbe huu utamfikia. Nilitaka atoe ufafanuzi alikuwa anamaanisha nini kwa kauli yake hii.

Waanza kupigiana debe wao kwa wao

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, asiyekuwa na wizara maalumu, Profesa Mark Mwandosya, amempigia debe Spika wa Bunge, Anne Makinda, akisema kuwa anafaa kuwa rais kutokana na sifa zake. Profesa Mwandosya alimwaga sifa hizo bungeni jana, wakati akiunga mkono Azimio la Bunge la kumpongeza Makinda, kutokana na kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA). Profesa Mwandosya, ambaye miaka ya nyuma alijitosa katika kinyang’anyiro cha urais, alisema Spika Makinda ana sifa zaidi ya kumi ambazo zinamtosheleza kuwa rais na kwamba ni watu wachache wenye sifa kama hizo. Akitaja sifa hizo, Profesa Mwandosya alisema Makinda ni mtu anayejiamini, mtenda haki, mchapakazi, mzoefu, msikivu, mbunifu, mwelewa, mvumilivu, mnyenyekevu na pia ni mtu mwenye msimamo. Alisema kutokana na sifa hizo, Makinda anafaa kuwa kiongozi wa ngazi ya juu katika nchi, huku akimtazama kuwa ni mwanamke tishio katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015. “Kwa namna ninavyomfahamu Spika Makinda ni tishio kwa uchaguzi wa rais mwaka 2015, kutokana na jinsi alivyokuwa na uwezo na mambo aliyowahi kulifanyia taifa hili. “Kuchaguliwa kwake kuwa rais wa CPA ni hatua muhimu na nzuri kwa wanawake wengi kuongezeka katika Bunge la mwaka 2015 kwa kufikia asilimia 55, kutokana na utendaji kazi wake uliotukuka,” alisema Profesa Mwandosya. Profesa Mwandosya, ambaye amekuwa serikalini kwa muda mrefu, mwaka 2005 alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuwania urais.Hata hivyo, kutokana na mchujo, Mwandosya alifanikiwa kuingia katika tatu bora. Wengine walikuwa ni Dk. Salim Ahmed Salim, Rais Jakaya Kikwete. Naye Mbunge wa Viti Maalum, Anna Abdallah (CCM), alimwaga sifa kwa kiongozi huyo wa Bunge na kusema kuwa ni mwanamke shupavu atakayekuwa tishio katika uchaguzi mkuu ujao. Akichangia mjadala huo wa kumpongeza Spika, Anna Abdallah, alisema Makinda ni mwanamke mwenye uwezo wa kuongoza nafasi yoyote ya juu, ikiwemo urais wa nchi. Alisema kutokana na uzoefu wake katika uongozi hapa nchini, ameweza kuaminika hata nje ya nchi, jambo ambalo limemfanya kuchaguliwa kuwa Rais wa CPA. “Kwa muda mrefu nchi yetu imekuwa ikihubiri juu ya mwanamke kupewa fursa na hasa kama ana uwezo, sasa wenzetu CPA wameweza kuliona hili wamemchagua,” alisema. Mbunge huyo aliwataka wanawake kutojali maneno ya pembeni na sasa ni lazima jamii ikubali kumuamini mwanamke kwa kumpa nafasi ya juu ya uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Awali akisoma Azimio hilo la Bunge, Mwenyekiti wa CPA-Tanzania, Mussa Azzan Zungu, alisema Spika Makinda alishika wadhifa huo baada ya kufanyika kwa mkutano wa 44 wa chama hicho. Zungu, ambaye ni Mbunge wa Ilala, alisema katika mkutano huo Bunge la Tanzania liliwakilishwa na wabunge wanane, akiwemo Spika Makinda na baadaye ulifanyika uchaguzi huo. Chanzo:Mtanzania

Ulaya:Arsenal na Man City wataweza?

Timu ya Arsenal wakati mgumu katika kombe la Klabu Bingwa
Timu ya Arsenal huenda ikawa na kibarua kigumu katika mechi za kutafuta nafasi ya kujitosa katika duru ya muondoano ya kombe la klabu bingwa bara ulaya.
Katika mechi za makundi vijana wa Arsene Wenger wamepangwa kundi moja na Borussia Dortmund ya Ujerumani, Olympic Marseille ya Ufaransa na Napoli kutoka Italy.
Arsenal waliingia katika duru ya makundi baada ya kuibandua timu ya Fenerbahce 5-0 katika mechi za mchujo zilizochezwa ugenini na nyumbani.
Timu nyegine ya Uingereza itakayo kuwa na wakati mgumu katika mechi hizo za makundi ni Celtic ya Scotland kwani imepangwa kucheza na mibabe ya soka Barcelona, AC Milan ya Italy na Ajax ya Uholanzi.
Jee Man City wataweza safari hii
Manchester City nao watalazimika kupepetana na bingwa wa kombe hilo la klabu bingwa ,Ulaya Bayern Munich, CSKA Moscow na Viktoria Plzen. Wapenzi wengi wa soka wanajiuliza je safari hii baada ya kupata kocha mpya mwenye uzoefu katika michuano hiyo ya kombe la klabu bingwa Manuel Pellegrini,Man City wataweza kupiga hatua na kuingia katika mechi za muondoano?
Kwa upande mwengine Kocha mpya wa Manchester United ,David Moyes hatakuwa na kazi kubwa sana kwani watapepetana na Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen ya Ujerumani na Real Sociedad ya Uhispania.
Miongoni mwa timu za Uingereza ni Chelsea peke yake ndio yenye kazi nyepesi kwani katika kundi lao watamenyana na Schalke ya Ujerumani, FC Basel na Steaua Bucharest.
Mechi za kwanza za makundi zinapaswa kugaragawa kati ya Septemba17-18 mwaka huu.

Orodha kamili ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya

Group A: Manchester United, Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen, Real Sociedad
Group B: Real Madrid, Juventus, Galatasaray, FC Copenhagen
Group C: Benfica, Paris St-Germain, Olympiakos, Anderlecht
Group D: Bayern Munich, CSKA Moscow, Manchester City, Viktoria Plzen
Group E: Chelsea, Schalke, FC Basel, Steaua Bucharest
Group F: Arsenal, Marseille, Borussia Dortmund, Napoli
Group G: Porto, Atletico Madrid, Zenit St Petersburg, Austria Vienna
Group H: Barcelona, AC Milan, Ajax, Celtic