Jumatatu, 21 Oktoba 2013

WAUMINI WASHAMBULIWA WAKITOKA KANISANI KWENYE SHEREHE ZA HARUSI HUKO MISRI



Waumini walishambuliwa wakiwa wanatoka kanisani

Watu watatu akiwemo msichana mdogo mwenye umri wa miaka 8 aliuawa wakati watu waliokuwa wamejihami wakiwa kwenye pikipiki kushambulia sherehe za ndoa nje ya kanisa la Kikopti mjini Cairo.
Takriban wengine 9 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo mjini Giza.
Hata hivyo hakuna taarifa zozote kuhusu nani aliyehusika na shambulizi hilo.
Jamii ya wakristo wa kikopti wamekuwa wakishambuliwa na baadhi ya waisilamu wanaotuhumu kanisa kwa kuunga mkono jeshi katika kumpindua aliyekuwa Rais Mohammed Morsi mwezi Julai.
Washambuliaji hao ambao hawakutambuliwa, waliwafyatulia risasi kiholela watu waliokuwa wanaondoka kanisani.

MAGAZETI YA LEO TAR 21.10.2013..TUME YA WALIOBA YAOMBA MUDA ZAIDI,WAZIRI WA KIKWETE AFANYA UCHOCHEZI,VYAMA VYAMTEGA ZITTO...USIKOSE

DSC 0057 aae29 DSC 0060 14b36DSC 0058 6a210DSC 0059 42743DSC 0061 32764DSC 0062 5a999DSC 0063 53a93DSC 0064 2bda4

ONA JINSI WANADAMU TUNAVYOISHI KWA TAABU NA MASHAKA

WANAFUNZI WAKIPAMBANA NA POLISI HUKO CAIRO MISRI
Mapambano mjini Cairo
Polisi wa Misri wamefyatua moshi wa kutoza machozi kuvunja maandamano mjini Cairo, ya wanafunzi wanaomuunga mkono rais wa zamani, Mohamed Morsi.
Mawe yalirushwa na pande zote mbili huku wanafunzi mia kadha wakijaribu kutoka chuoni kuelekea Medani ya Rabaa, pahala pa kambi ya wafuasi wa Morsi ambayo ilifungwa na wakuu miezi miwili iliyopita.
Hii ni siku ya pili ya mapambano katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, ambako kuna wafuasi wengi wa chama cha Muslim Brotherhood cha Bwana Morsi.
Bwana Morsi aliondolewa madarakani na jeshi mwezi wa Julai.

BOKO HARAMU WAWAUA MADEREVA 19 NIGERIA
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/10/15/131015124213_nigeria_bokoharam_304x171_afp.jpg 
Mabaki ya magari ya madereva waliouawa na Boko Haram

Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa wameweka kukagua magari katika jimbo la Borno.
Wanaume hao waliokuwa wamejihami , waliwasimamisha madereva na kuwaamrisha kuondoka kutoka katika magari yao kabla ya kuwapiga risasi na kuwaua.
Walioshuhudia tukio hilo waliambia BBC kuwa wanaume hao walikuwa wanachama wa Boko Haram, ingawa kundi hilo bado halijatamka chochote kuhusu mauaji hayo.
Jimbo hilo la Kaskazini mwa Nigeria liko chini ya sharia ya hali ya hatari, huku Boko Haram wakiwa vitani na serikali kutaka utawala wa kiisilamu.
Kundi hilo huwalenga raia na wanajeshi kwa mashambulizi ikiwemo shule na makabiliano ya mara kwa mara na jeshi la taifa.
Shambulizi la hivi karibuni, lilifanyika Jumapili, asubuhi karibu na mji wa Logumani, ambao hauko mbali sana na mpaka na Cameroon.
Walionusurika shambulizi hilo walisema kuwa washambuliaji walivaa nguo za jeshi na walikuwa wanaendesha pikipiki kabla ya kuwashambulia waathiriwa.
"Takriban wanaume 9 walituamuru kuondoka kwenye magari yeu na kulala chini,’’ alisema mwanamume
"Waliwaua watu 5 kwa kuwapiga risasi na kasha kuwanyonga wengine 14 kabla ya mtu mmoja kuwapigia simu na kuwambia kuwa wanjeshi wanakuja.’’
Alisema washambuliaji baadaye walitoroka na kujificha msituni kwa pikipiki zao.
Manusura mwingine alisema kuwa alisikia mtu aliyekuwa karibu naye akiuawa kwa kisu. Alisema ana uhakika kuwa washambuliaji walikuwa Boko Haram kwa sababu ya kuwa na ndevu.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo alisema kuwa ni jambo la kawida kwa polisi kuweka vizuizi barabarani hasa katika maeneo yenye misukosuko na huenda washambuliaji waliiga mbinu hioyo ya jeshi ili kuwanasa waathiriwa. I,
Boko Haram limezua mgogoro mkubwa wa kisiasa Nigeria tangu mwaka 2009, nia yao kuu ikiwa kuunda utawala wa kiisilamu, hasa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi
Kundi hilo limelaumiwa kwa mashambulizi kadhaa ambao yamesababisha takribna vifo 2,000 tangu mwka 2011.