Jumanne, 31 Desemba 2013

NCHI YA MISRI NAYO ILIKUMBWA NA MISUKOSUKO YA HATARI MWAKA 2013

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/12/13/121213160413_egypt_sergey_ponomarev_976x549_sergeyponomarev.jpg 
Wanajeshi wa Misri wanashika doria katika baadhi ya miji mikubwa ambapo maandamano yanafanyika kupinga au kuunga mkono kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba itakayofanyika siku ya Jumamosi
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/12/13/121213152614_egypt_sergey_ponomarev_976x549_sergeyponomarev.jpg
Wanajeshi wameruhusiwa kuchukua hatua dhidi ya waandamanaji watakaozua rabsha 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/12/13/121213152724_egypt_sergey_ponomarev_976x549_sergeyponomarev.jpg 
Katika mji wa Alexandria ambao ni mji wa bandarini , wananchi asubuhi ya leo walianza kuandamana kuipinga katiba lakini polisi walikuwepo kuwazuia
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/12/13/121213152807_egypt_sergey_ponomarev_976x549_sergeyponomarev.jpg
Maandamano yalianza baada ya mhubiri mmoja katika msikiti mmoja kuwashauri waumini kupigia kura ya ndio katiba 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/12/13/121213152850_egypt_sergey_ponomarev_976x549_sergeyponomarev.jpg
Waandamanaji mahasimu hawajachoka tangu mapema wiki hii walipoanza kuandamana wakipinga katiba ya rais Morsi huku wengine wakiiunga mkono
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/12/13/121213153352_egypt_sergey_ponomarev_976x549_sergeyponomarev.jpg
Waandamanaji wengi wanasema kuwa wataipinga katiba hiyo
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/12/13/121213155901_egypt_sergey_ponomarev_976x549_sergeyponomarev.jpg
Hawakutaka kuondoka hata baada ya jeshi kuamrishwa kuwakamata wale watakaokiuka sheria, agizo ambalo wengi wamelitafsiri kama Misri kurejea katika enzi ya kidikteta
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2012/12/13/121213161104_egypt_sergey_ponomarev_976x549_sergeyponomarev.jpg
Wengi walikesha katika medani ya Tahrir kuelezea kero lao dhidi ya katiba mpya

JE, UNAIKUMBUKA HII SIKU AMBAPO PAPA BENEDICT WA XVI ALIAGWA RASMI NA WAUMINI WA KIKATOLIKI DUNIANI?

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227150951_st_peters_sq_getty.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227150949_rosary_reuters.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227150944_pope_afp.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227150942_popemobile_afp.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227150940_pope_3_reuters.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227150938_flag_afp.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227141257__66099839_66099838.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227150934_banner_reuters.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/02/27/130227150936_cardinals_getty.jpg 
 
ENDLEA KUFUATILIA MATUKIO ZAID YA HAYA KWA MWAKA 2013
 

HII ILITOKEA HUKO OKLAHOMA AMBAPO WATOTO TAKRIBANI 20 WALIPOTEZA MAISHA

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521041411_oklahoma_01_ap_g976.jpg 

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521082602_oklahoma_tornado_976x549_reuters.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521043411_oklahoma_tornado_6_.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521055539_tornado_oklahoma_976x549_reuters.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521082005_oklahoma_tornado_976x549_ap.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521082152_oklahoma_tornado_976x549_ap.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521082259_oklahoma_tornado_976x549_getty.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521082344_oklahoma_tornado_976x549_reuters.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521082429_oklahoma_tornado_976x549_reuters.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521082525_oklahoma_tornado_976x549_reuters.jpg 
 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521003743_sp_galeria_oklahoma6_976x549_reuters.jpg

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/05/21/130521003530_sp_galeria_oklahoma2_976x549_ap.jpg 
 
JE UNA KIPI CHA KUISHAURI BLOG HII KIBORESHWE KWA AJILI YA KUENDELEA KUKUHABARISHA HAPO MWAKA 2014?


MOJA YA MATUKIO YA KUSIKITISHA SANA KWA MWAKA 2013 NI MAUAJI YA NGOME YA HEZBOLLAH

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115932_blast_afp-1.jpg 
Takriban watu 22 wameripotiwa kufariki katika milipuko miwili ambayo ililenga ubalozi wa Iran mjini Beirut, mji mkuu wa Lebanon
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115934_blast_afp-2.jpg
Afisaa mmoja mkuu katika ubalozi huo Ebrahim Ansari alikuwa miongoni mwa waliofariki. Maafisa wamesema kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115936_blast_ap-3.jpg
Picha nyingi za mashambulizi hayo zilionyesha magari yakiteketea pamoja na miili ya watu ikiwa imetapakaa kwenye barabara za eneo hilo. Majumba pia yaliharibiwa vibaya
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115938_blast_ap-4.jpg
Iran inaunga mkono kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Hezbollah ambalo limewapeleka wapiganaji nchini Syria kuunga mkono serikali ya Rais Bashar al Assad. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115940_blast_afp-5.jpg
Duru zinasema kuwa moja ya milipuko hio, ilisababishwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga, wakati shambulio la pili lilitokana na bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari. 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115942_blast_reuters-6.jpg
Shirika la habari la Reuters linanukuu kituo cha televisheni cha CCTV, kikionyesha mwanamume mmoja akikimbia kutoka katika ubalozi wa Iran na kisha kujilipua
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115944_blast_reuters-7.jpg
Balozi wa Iran nchini Beirut alithibitisha kifo cha bwana Ansari, ingawa haijulikani ikiwa alikuwa ndani ya ubalozi au katika jengo jirani 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2013/11/19/131119115946_blast_ap-8.jpg
Syria imelaani vikali mashambulizi hayo. Mgogoro wa kisiasa nchini Syria umechochea kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini Lebanon. 

HAYA NI BAADHI TU YA MATUKIO AMBAYO FREE MEDIA TO BLOGS INAJARIBU KUKUHABARISHA

Ijumaa, 27 Desemba 2013

HABARI PICHA...!

WAKAZI WA MBEZI MWISHO WAKICHAGUA MITUMBA BARABARA YA DAR-MOROGORO
SHIMO HILI LIKO STENDI YA MWENGE SERIKALI IMELIFUMBIA MACHO NA KULIACHA KUENDELEA KUWA HATARI KWA WAKAZI WA ENEO HILO
ASKOFU DR ALEX MALASUSA AKIWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA KRISMAS  WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM
 

Jumatano, 25 Desemba 2013

WAKATI NYIE MNAKULA NA KUSHEREKEA SIKUKUU YA CHRISMAS ONA WENENU SUDANI KUSINI

Raia wa Sudan Kusini 
Huku Umoja wa Mataifa ukijiandaa kutuma maelfu ya wanajeshi zaidi wa kutunza amani Sudan Kusini, viongozi wa jamii ya kimataifa wanaendelea kutoa wito wa kusitishwa mapigano yanayoendelea nchini humo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ametoa wito kwa rais wa Sudan Kusini, Salva Kirr, na aliyekuwa makamo wake, Salva Kirr, kuanzisha mazungumzo ya amani.
Uchina pia imetoa wito kuwa mapigano yasitishwe.
Kuna taarifa kwamba kumetokea mapambano Malakal, mji mkuu wa jimbo la mafuta la Upper Nile state.
Wanajeshi wa serikali wanasema wameukomboa mji muhimu wa Bor.
Mwandishi wa BBC anasema haikuelekea kuwa ghasia zitamalizika karibuni - ghasia zilizozidisha uhasama wa kikabila na kupelekea maelfu kuhama makwao.
 

Jumanne, 24 Desemba 2013

HALI HII SUDANI KUSINI MPAKA LINI? MAUAJI KILA KONA

 
Waathirika wa mapigano Sudan Kusini
Taarifa mpya zimeibuka zikieleza kuwepo kwa mauaji ya kikabila yaliyofanyika katika kipindi cha zaidi ya wiki moja ya ghasia nchini Sudan Kusini.
Mwandishi wa habari mmoja kutoka mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, amewakariri watu walioshuhudia mauaji hayo wakisema zaidi ya watu 200, wengi wao wakitoka kabila la Nuer , wameuawa kwa kupigwa risasi na majeshi ya usalama.
Mtu mwingine kutoka Juba amesema watu wenye silaha kutoka kabila la Dinka walikuwa wakiwashambulia kwa risasi watu kutoka maeneo ya Nuer.
Ghasia hizo zimekuja huku kukiwa na hali ya kugombea madaraka kati ya Rais Salva Kiir, kutoka kabila la Dinka, na aliyekuwa naibu wake Riek Machar kutoka kabila la Nuer.
Serikali ya Sudan Kusini imekanusha kuhusika na ghasia za kikabila.
Taarifa hizo zimekuja wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuongeza askari 5,500 wa Umoja wa Mataifa katika kikosi cha askari 7,000 wa Umoja wa Mataifa waliopo Sudan Kusini.
Waasi wanaomuunga mkono makamu wa rais aliyefukuzwa Riek Machar walitwaa miji mikubwa wiki iliyopita.
Maelfu ya watu wamekimbia mapigano.
 

MLIPUKO WAPIGA JENGO LA USALAMA MISRI

 
Mlipuko waharibu sehemu ya jengo la usalama Misri
Mlipuko mkubwa katika jengo moja la usalama kaskazini mwa Misri umesababisha watu wapatao 14 kuuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Maafisa nchini humo pamoja na vyombo vya habari vya serikali wamesema, mlipuko huo, ambao umeripotiwa kusababishwa na bomu lililotegwa katika gari, umesababisha kuporomoka sehemu ya jengo hilo katika mji wa Mansoura.
Waziri Mkuu wa Mpito Hazem Beblawi ameelezea tukio hilo kama "kitendo cha ugaidi".
Mashambulio dhidi ya majeshi ya usalama na polisi nchini Misri yameongezeka tangu jeshi nchini humo limtoe madarakani rais wa Kiislam Mohammed Morsi mwezi Julai, 2013.
Mpaka sasa hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulio hilo.
Bwana Beblawi amekiambia kituo cha televisheni cha ONTV: "Serikali itafanya kila iwezalo kuwasaka wahalifu wote waaliotekeleza, kupanga na kusaidia kufanyika kwa shambulio hilo."
Athari za mlipuko huo zilipatika katika maeneo ya umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.
Televisheni ya Misri imewaomba watazamaji wake kwenda hospitali kutoa damu.
Kikundi cha Muslim Brotherhood - kinachomuunga mkono Bwana Morsi na kilichopigwa marufuku na serikali ya mpito ya Misri, kimelaani shambulio hilo.
"Muslim Brotherhood kinachukulia kitendo hiki kama shambulio la moja kwa moja katika umoja wa watu wa Misri," kimesema katika taarifa yake.

Mkuu wa usalama amejeruhiwa'

Mlipuko huo ulipiga jengo hilo Jumatatu usiku wa manane.
Zaidi ya watu 100 walijeruhiwa. Taarifa za vyombo vya habari zinasema mkuu wa usalama wa jimbo ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa.
Mlipuko huo ulivunja vioo vya madirisha ya majengo jirani na athari zake kufika umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.
Mansoura - mji wenye idadi ya watu 480,000 - ni makao makuu ya mkoa wa Dakahliya katika jimbo la Nile Delta.
Tangu kuondolewa madarakani kwa Bwana Morsi - rais wa kwanza wa Misri aliyechaguliwa kwa njia za kidemokrasia - wafuasi wake wamekuwa wakiandaa maandamano makubwa wakitaka kuachiliwa huru kwa kiongozi wao.
Zaidi ya wanachama 2,000 wa Muslim Brotherhood wamekamatwa, na 450 kati yao, siku ya Jumatatu walianza mgomo wa kususia chakula wakipinga kudhalilishwa.".
Bwana Morsi kwa sasa anakabiliwa na kesi tatu tofauti za uhalifu zikihusishwa na nafasi yake akiwa madarakani.
Kesi ya kwanza ilifunguliwa tarehe Novemba, lakini imeahirishwa hadi Januari 8, 2014.

Jumatatu, 23 Desemba 2013

HII NDIYO AJALI YA TRENI ILIYOTOKEA KIBERA HUKO NAIROBI KENYA

Vibanda vya Kibera vimejengwa karibu sana na njia ya reli
Waokozi wana wasiwasi kuwa pengine watu kadha wamenasa chini ya treni iliyopinduka katika mitaa ya Kibera, Nairobi - eneo la watu maskini.
Watu kama kumi walijeruhiwa wakati mabehewa mane ya mizigo yalipopinduka juu ya vibanda kando ya njia ya reli.
Waokozi wanajaribu kutafuta nafasi katika mtaa wenye nyumba zilizogandana sana, ili kuleta mashini ya kunyanyua mabehewa ili kuwafikia wale walionasa.
Mabehewa yalianguka juu ya vibanda vilivyo karibu na njia ya reli.
Magazeti yanaarifu kuwa kazi za uokozi zimezingika kwa sababu watu wengi wamezonga eneo hilo.