Jumatatu, 14 Julai 2014

TAZAMA MAISHA YA WAAFRIKA NCHINI BRAZIL WALIOHAMIA KUTOKANA NA KOMBE LA DUNIA 2014

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082159__76151744_africansinbrazil01.jpg 
Brazil ni nchi yenye urathi mkubwa wa kiafrika , na ni kwa sababu ya historia biashara ya utumwa. Mamilioni ya watu nchii Brazil wana asili ya kiafrika. Lakini je maisha yako vipi kwa waafrika waliohamia nchini humo aidha kufanya kazi au kusoma? Mwandishi wa BBC Manuel Toledo alikuwa nchini Brazil na alikutana na baadhi yao.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082201__76151745_africansinbrazil02biyou_zrestaurant.jpg 
Victor Macaia (katikati) na mkewe Melanito Biyouha, wanatoka nchini Cameroon. Walifungua mgahawa wao wa chakula cha kiafrika mjini Sao Paulo miaka sita iliyopita. "mwanzoni asilimia 80 ya wateja wetu walikuwa waafrika, lakini sasa asilimia 90 ni wageni na wenyeji wa-Brazil. Chakula chetu chote ni cha kiafrika,'' alisema mwanamume huyo.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082203__76151748_africansinbrazil03biyou_zrestaurant.jpg 
ilikuwa vigumu sana kwetu kaunza biashara hii. Wakati mwingine huna nyaraka zinazotakikana, pesa na gharama au hata uzoefu wa kazi. Inachukua muda, kufanya kazi muda wa kupitia masaibu na pia muda wa kupata faida. Lakini sasa tuko vizuri sana,'' Bwana Macaia aliongeza kusema.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082216__76153510_africansinbrazil04alefallsowsenegal.jpg 
Ale Fall Sow, kutoka Senegal ni mhadhiri katika chuo kikuu Brasilia. '' Nimeishi nchini Brazil kwa miaka 26. Nilikuja hapa kwa mara ya kwanza kama mwanafunzi. Mke wangu na watoto wangu ni wa-Brazil. Wanapenda Afrika na wao huenda huko kwa likizo mara kwa mara.  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082205__76152027_africansinbrazil05tresormuteba.jpg 
Nchini Brazil kuna asili mbali mbali. Kwa sababu za kihistoria, kuna watu weusi Kaskazini mwa nchi,'' asema mwanafunzi Tresor Mukendi Muteba, kutoka Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo. Nahisi kama niko nyumbani hapa. Utamaduni wa Brazil unafanana na utamaduni wa Afrika. Kwa sababu ya hilo, wakati mwingi mimi huhisi kama niko Afrika. ''  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714091056_brazil_afrika_976x549_bbc_nocredit.jpg 
"nimekuwa nchini Brazil, kwa miezi mitatu au minne, asema Uju Juliana kutoka Nigeria. "Brazil ni mahala pazuri sana. Wanawake wa kiafrika sisi huhisi kama tuko tu nyumbani. Ningesema kwamba hapa Brazil watu huheshimu wanawake zaidi hata kuliko nchini mwangu. ''  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714091140_brazil_afrika_976x549_bbc_nocredit.jpg 
Lacine Sanogo kutoka Ivory Coast anasema: "nilikuja hapa kucheza soka. Lakini maisha hapa ni magumu hasa kwetu raia wa kigeni. Hatupewi nafasi za kutosha, Nimekuwa nikicheza katika ligi ya daraja ya pili lakini hivi karibuni nilipata jeraha la goti. Ambavyo soka inachezwa Afrika ni tofauti sana na inavyochezwa hapa. Nimejifunza mambo mengi. ''  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082218__76153511_africansinbrazil08elhadjiomar.jpg 
El Hadji Omar, kutoka Senegal anauza mali yake barabarani. "nilikuja Brazil miezi miwili iliyopita kutafuta kazi. Sijui nitakuwa hapa kwa muda gani lakini naipenda nchi hii. Kama katika sehemu nyingine yoyote duniani, kuna watu wazuri na wabaya. Lakini watu nchini Brazil ni kama tu sisi waafrika. ''  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082210__76152141_africansinbrazil07yussifmuhktar.jpg 
nimekuwa hapa kwa miezi minne,'' asema Yussif Muhktar kutoka Ghana. "nilikuja hapa kufanya kazi. Wa-Brazil ni watu wazuri sana na wanapenda kila mtu na ninashukuru kwa hilo. ''  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082332__76154617_africansinbrazil09sergetchieguen.jpg 
Serge Tchieguen kutoka Cameroon anasema: "ninafanya kazi ya usimamizi wa michezo, na hiyo ni sekta ambayo imekomaa sana hapa Brazil. Nimejifunza mengi. Nadhani nimebadilika na kuwa bora zaidi tangu kuja hapa miaka minne iliyopita kwa namna ambavyo nafikiria na pia kufanya kazi. ''  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/14/140714082214__76152320_africansinbrazil11ifeanyiokafor.jpg 
Ifeanyi Okafor, kutoka Nigeria, ni mhandisi katika kampuni ya kuchimba mafuta. "ninaishi eneo linaljulikana kama Macae karibu na Rio de Janeiro. Nimeishi hapo kwa miaka miwili. Ni mara ya kwanza kwangu kufanya kazi nje ya Afrika. Nimefurahi sana na nina marafiki wengi sana hapa Brazil.''  


endelea kufuatilia matukio mbalimblia kupitia blog yako ya kijanja
 

BADO HAIJULIKANI NI LINI WATOTO WAKIKE WA NIGERIA WATAPATIKANA

 

Malala akutana na Rais Goodluck Nigeria

Malala na mmoja wa wazazi wa wasichana waliotekwa nyara Nigeria

Mwanaharakati mwenye umri mdogo raia wa pakistan Malala Yousafzai amekutana na rais wa Nigeria Goodlack Jonathan mjini Abuja.
Lengo la mkutano huo ilikuwa kwa Malala kushinikiza Rais Goodluck kuchukua hatua zaidi ili kuwakoa wasichana wa shule waliotekwa na kundi la wanmgambo wa Boko Haram mwezi April.
Tayari mwanaharakati huyo ashakutana na familia za wasichana hao kuwapa moyo na matumaini.
Boko Haram wametoa kanda ya video ya kusuta kampeni za kutaka kuachiliwa wasichana hao. Kundi limetaka kuachiliwa kwa wapiganaji wake.
Malala alipigwa risasi kichwani na kundi la Taliban nchini Afghanistan alipokuwa akipigania elimu kwa wasichana.
Malala mwenyewea alikuwa mwathiriwa wa vita vya Taleban nchini Pakistna ambao na wao pia wanapinga elimu kwa watoto wasichana.
Yuko nchini Nigeria kwa ziara ya siku tatu. Katika siku ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, ameamua kwenda Nigeria kutoa wito wa kuwachiliwa kwa wasichana hao wengi ambao wana umri sawa na yeye, miaka 17.
Ni miezi mitatu tangu wasichana hao zaidi ya 200 kutekwa nyara na pia sio kawaida kwamba Rais Jonathan bado hata hajakutana na familia za wasichana hao.
 

Jumapili, 13 Julai 2014

LEO KATIKA MATUKIO YA PICHA

LIVE MUDA HUU: KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 75 YA KANISA LA TAG, UWANJA WA SOKOINE MBEYA. MGENI RASMI NI RAIS DK. JAKAYA KIKWETE.













Picha na Mbeya yetu Blog

Endelea kufuatilia hapa

HII NI ZAIDI YA UJUAVYO....UGONJWA WA EBOLA NI JANGA KWA AFRIKA HASA MAGHARIBI

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131439__75930220_msb8380_medium.jpg 
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetaka "hatua za dharura" zichukuliwe ili kudhibiti kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Africa magharibi, ambao umewauwa zaidi ya watu 400. Ugonjwa huu ndio mkubwa zaidi duniani kuzuka kutokana na visa vyake, vifo na kusambaa katika maeneo.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131441__75930223_msb8345_medium.jpg
Kumekuwepo na visa visivyopungua 600 nchini Guinea - ambapo ugonjwa huo ulianza kuzuka miezi minne iliyopita mjini Guekedou, ambao ulikuwa kituo kikubwa cha biashara, kilichowavutia wauzaji na wanunuzi kutoka mataifa kadhaa.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131446__75930386_msb8353_medium.jpg
Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres (MSF) tayari limeonya kuwa kusambaa kwa ebola hakuwezi kudhibitiwa. Shirika hilo lina wafanyikazi 300 wa kimataifa na vile vile wa kitaifa wanaofanya kazi nchini Guinea, Sierra Leone pamoja na Liberia, ambako ugonjwa huo unaenea kwa kasi. Mataifa mengine yako 
macho iwapo ugonjwa huo utasambaa Zaidi.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131523__75931214_msb8358_medium.jpg
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Ebola ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na ambao dalili zake za mwanzo huweza kuwa kushikwa na homa, kuwa dhaifu, kuumwa na misuli na kuumwa na koo. Na huo ni mwanzo tu: kile kinachofuata ni kutapika, kuendesha na -wakati mwingine- kuvuja damu.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131458__75930623_msb8400_medium.jpg
Virusi hivyo huenea kwa haraka sana, na hadi sasa hakuna dawa inayotambulika kuweza kuvitibu, kwa hivyo wanaotoa huduma za matibabu huvalia mavazi yanayowakinga kutokana na kuambukizwa kwa ugonjwa huo. Kulingana na uzito wa athari za ugonjwa huo, hadi kufikia asilimia 90 ya walioambukizwa huaga dunia. Anayehakikisha usafi anawakaribia wagonjwa wanaosubiri matokeo baada ya kupimwa damu.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131456__75930581_msb8385_medium.jpg
 Vipimo vya maabara vitaonyesha kwa saa kadhaa iwapo sampuli ya damu inayopimwa ina virusi vya Ebola au la.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131450__75930518_msb8378_medium.jpg
Baada ya kukumbana na virusi hivyo katika sehemu iliyotengwa, mavazi na viatu husafishwa kwa Chlorine.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131443__75930225_msb8344_medium.jpg
Kando na kutoa huduma za kliniki, kikundi hicho hutoa hamasisho kuhusu ugonjwa huo. Hapa Touloubengo, familia tano ambazo nyumba zao zilikuwa zimesafishwa siku kadhaa zilizopita kutokana na kuaga dunia kwa mmoja wao wanakabidhiwa magodoro.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131448__75930451_msb8366_medium.jpg
Sio kila mtu aliye salama. Hapa familia ya Kinda Marie Kamano, akiwemo dadake (katikati), pamoja na wanajamii wengine wanahuzunika katika mazishi yake karibu na nyumba yake.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131453__75930538_msb8381_medium.jpg 

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/02/140702131500__75930666_msb8383_medium.jpg 
Takriban watu 600 wamefariki kutokana na homa ya Ebola Afrika Magharibi


Endelea kufuatilia
 

Jumamosi, 12 Julai 2014

Duniani kote tunatakiwa kuomba amani ilejee

 
Miili ya Wapalestina waliouawa kwa mashambulizi yanayofanywa na Israel
Umoja wa Mataifa umesema robo tatu ya Wapalestina waliouawa kwa mashambulizi ya ndege yanayoendelea yanayofanywa na Israel huko Gaza ni raia wa kawaida.
Maafisa wa Palestina wanasema raia mia moja ishirini wameuwawa tangu mashambulio kuanza.
Magari ya deraya yakiwa vitani
Israel imesema inafanya mashambulio hayo, ili kujaribu kuwazuia wapiganaji wa Hamas, ambao wamekuwa wakirusha mamia ya makomborakwenye ardhi ya Israel.
Israel inalaumu wapiganaji wa Hamas kwa kutumia raia kama ngao kwa kuweka vifaa vya kivita kwenye makazi ya watu.
Professor Manuel Hassassian mwakilishi wa Palestina nchini Uingereza, ameiambia BBC, Israel kwa kuwalenga Hamas hukutakwepa kuwadhuru raia.
Alisema idadi kubwa ya raia wamekufa siyo sababu Hamas inajificha kati ya raia, yaani inawatumia raia kama kinga.
Gaza, kwa hivo wanapowalenga Hamas kamawanavosema, wanawalenga wa-Palestina wote. Siyo Gaza peke yake.Katika Ufukwe wa Magharibi piya, Israil imekuwa ikiwauwa kiholela, na huko hakuna makombora yaliyolegwa dhidi ya Israil" Alisema Hassassian.

Alhamisi, 10 Julai 2014

HII NI ZAIDI YA MVUA YA MAGOLI: KICHAPO KWA TIMU YA BRAZIL

http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/09/140709084904_bra_v_ger_1.jpg 
Bao la kwanza la Ujerumani lilipokewa kwa vifijo na nderemo na mashabiki waliokuwa wamejaa pomoni kushuhudia timu yao ikimenyena na mabingwa mara sita wa kombe la dunia Brazil  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/08/140708203553_thomas_mueller_976x549_reuters.jpg 
Mechi hii ilikua ya kwanza ya nusu fainali katika kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil  
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/08/140708204203_toni_kroos_976x549_afp.jpg 
Wengi wamesema wachezaji wa Ujerumani walikuwa 'balaa' yaani walikuwa wakali katika mechi hiyo
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/08/140708225505_brazil_defeat_976x549_ap.jpg
Kipa wa Ujerumani hakuwa na chochote cha kufanya kwani hali ilikuwa ngumu kweli.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/09/140709084918_bra_v_ger_8.jpg
Ilikuwa sherehe kila pembe ya dunia kutoka kwa mashabiki wa Ujerumani na hata nyumbani baada ya timu yao kuingiza mabao matano katika dakika za kwanza 29 za mechi hiyo 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/08/140708203937_toni_kroos_976x549_reuters.jpg
Mabao yaliendelea kuingizwa hadi yakafika saba mwishoni mwa mechi. Brazil hata hivyo walikomboa bao moja la kupanguzia machozi, ila halikutosha kuondoa aibu waliyoipata katika mchuano huu ambao umewaacha wengi vinywa wazi
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/09/140709084910_bra_v_ger_4.jpg
Mashabiki wa Brazil walikuwa wanajionea giza uwanjani magoli yakiingizwa na Ujerumai kutoka pembe zote za uwanja
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/08/140708203223_thomas_mueller_976x549_ap.jpg
Ujerumani sasa watajiandaa kumenyana na mshindi wa mechi kati ya Uholanzi na Argentina Brazil itasalia kupigania nafasi ya tatu 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/09/140709084914_bra_v_ger_6.jpg
Huzuni ulitanda Brazil na kote duniani kwa mashabiki wa Brazil 
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/09/140709081157_david_luiz_brazil_football_worldcup_semi_final_976x549_reuters_nocredit.jpg
Lakini nahodha wa muda wa Brazil David Luiz amewataka mashabiki wa timu hiyo kote duniani kuwasamehe wachezaji waliokuwa uwanjani Selecao,walipoadhibiwa kichapo cha mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
http://wscdn.bbc.co.uk/worldservice/assets/images/2014/07/08/140708205601_germany_976x549_afp.jpg
Kwa sasa hadi fainali za kombe la dunia ni sherehe kote kote nchini Ujerumani 

ENDELEA KUFUATILIA MATUKIO ZAIDI YA KOMBE LA DUNIA KUPITIA HAPAHAPA BLOG YA KIJANJA
NITAWALETEA TENA MATUKIO YA BRAZIL KUTAFUTA NAFASI YA TATU AMA YA NNE!