Ijumaa, 14 Agosti 2015
Jumanne, 28 Julai 2015
MATUKIO KATIKA PICHA...SIASA SIYO UGOMVI NI KUZIDIANA KETE TU
Dkt Magufuli akiwa na mbowe hii inaonyesha kuwa mbowe anakubali mziki wa magufuli mpaka kashindwa kujizuia kapanda gali moja na Dkt Magufuli.
Endelea kufuatilia kupitia blog ya kijanja
MZIMU WA AJALI ZA BARABARANI UNAENDELEA KUTUMALIZA...EEE MUNGU TUSAIDIE
Watu wanne wanasadikiwa kufariki dunia baada ya Basi la Kampuni ya Sabuni Express linalofanya safari zake kati ya Karagwe na Mwanza kugongana uso kwa uso na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser iliyokuwa imebeba Masister eneo la Bugorora,ikitokea Bukoba mjini kuelekea Mutukura.
Chanzo na mwandishi wa ITV na Radio One
SIASA NI MCHEZO MCHAFU....UKISEMA WA NINI WENZIO WANASEMA WATAMPATA LINI?
Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now.
Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: k
wa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais???
Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010.
Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma.
Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach.
Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.
endelea kufuatilia
Jumapili, 12 Julai 2015
Urais CCM........Magufuli Apata Ushindi wa Kishindo
Chama cha mapinduzi, CCM kimemteua Dr .Magufuli kuwa mgombea wa Urais 2015. Uteuzi wa Dr. Magufuli umetokana na ushindi wa kishindo alioupata baada ya mkutano mkuu kukutana jana usiku kwa ajili ya kupiga kura ili kupata jina...oja kati ya matatu yaliyokuwa yamependekezwa na Halmashauri kuu ya CCM.
Matokeo ni kama ifuatavyo
1.Magufuli.....87%
2. Amina.......10%
3.Migiro......3%
Jumamosi, 11 Julai 2015
CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO TAZARA MBEYA SACCOS LTD KIMETOA MIKOPO KWA WANACHAMA WAKE YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 60
WAFUATAO NI BAADHI YA WANACHAMA WALIONUFAIKA NA MIKOPO HIYO.
Bwana Yusto Barnabas (kushoto)
Bi.Teddy Ndimbo
Bwana Luka Mahenge (kushoto)
Bi. Bupe Kalinga
Bwana. Godfrey Mwakalindile (Kulia)
Bi. Rose Mwandiwa (Kulia)
Bi. Erikanali Nyari..(Kulia) akiwa badala ya Deborah Nyari
Bi. Salome Magwaza (katikati)
Endelea kutembelea blog hii kwa habari zaidi
HABARI KUBWA LEO-CCM KUMFIA KIKWETE WIKI HII?.MIPANGO YA KUASI CCM YAVUJA NI YAWASAKA URAIS,SOMA HAPO KUJUA
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika hivi karibuni picha na maktaba. |
HATMA ya Chama cha Mapinduzi CCM kuendelea salama au kufikia tamati na kuingia kwenye mpasuko mkubwa kutokana na Makada wake wanaotaka Urais ndani ya Chama hicho ni itabianika wiki hii.(Mtandao huu unaripoti) anandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Baada ya Kamati kuu ya chama hicho CC kinachotarajiwa kukutana Alhamisi ya Terehe 9 ya wiki hii ambapo kwa mujibu ya Ratiba ya chama hicho inaonyesha pamoja na mambo mengine kamati itakuwa na jukumu moja tu la “Kufyeka” majina ya takribani 38 ya makada walioomba ridhaa ya kutaka urais kwenye Chama hicho na kubakisha majina matano.
Taarifa kutoka ndani ya CCM zinasema kwa sasa chama hicho kipo kwenye presha kubwa kutoka kwa makada wake ambao wamejiapiza kwa udi na Uvumba lazima wapite na kuwa Mgombea wa Urais ambao taarifa zinasema Makada hao wanaojiapiza ni wale wanakubwa na Kashfa za ufisadi pamoja na kukiuka kanuni za chama.
Makada hao wakiongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa Ufisadi wa Kampuni ya tata ya kufua Umeme ya Richmound Edward Lowassa ambaye mara kwa mara kupitia Kambi zake kwamba akisema “hakuna wakulita jina lake ndani ya CC”
Mbali na Lowassa Kada mwengine wa CCM ambaye amekuwa akijiipiza pia hakuna wakulikata jina lake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimatifa Benard Membe ambapo naye amekuwa ajisifu kuwa lazima apite na kuwa Rais.
Kwa Mujibu wa Vyanzo vyetu vilivyopo ndani ya CCM zinasema kwa sasa chama hicho,kimekuwa na Presha kubwa ambapo kwa sasa wanatafakari ni njia gani watatumia kuwachagua wagombe ambapo watakiaacha chama hicho salama,
“Yaani wiki hii ndio chama chetu kitakuwa salama au ndio kitameguka maana kwa sasa chama kimekuwa na makundi makubwa sana ambayo kusema kweli hata kamati kuu sijui itakuja na jibu gani,ukitazama kuna makada wengi wamekubwa na kashfa kubwa za ufisadi wamekuwa ana nguvu tena wamepanga hata kufanya uasi endapo majina yao yatakatwa”
Taarifa zanasema Kada ambaye amekuwa akiogopesha Chama hicho ni Edward Lowassa ambapo kwa sasa amekuwa na Nguvu kubwa sana ndani ya chama hicho kutokana na mipango ambaye ameiandaa,
“Huyu bwana kusema kweli basi tena hawamuwezi,maana amekuwa na makundi makubwa ndani ya chama chetu amewanunua wajumbe wa Mkutano mkuu kwa pesa nyingi sana,yaani amevunja kanuni ya wazi za chama,amejigeuza kama kiongozi mkuu wa chama,yaani mapaka sasa chama kinamwogopa sana”
Kwa mujibu taarifa kutoka kambi ya Lowassa zinasema kwa sasa wamepanga hata kufanya “uasi”endapo kamati kuu ya CCM wakimkata mgombea wao.
“Sisi tunangojea kwa hamu siku hiyo ya tarehe 9 ndugu,ndio utaona makubwa hapa nchini,yaani tunajua kwenye kamati ya CC kunawatu hawamtaki Lowassa na wamepanga kumkata jina lake,nakuhakikishia hatukubali na ukitaka kuamini ngojea uone”
Kwa mujibu wa ratiba ya CCM inaonyesha baada ya kamati kuu ya ccm kupendekeza majina matano,kinachofuata ni Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM nayo itayakata majina mawili kati ya matano na kubakiza majina matatu ambayo yanapigiwa kura siku ya tarehe 11 na 12 ya jumamosi na jumapili na kupatikana mgombea Mmoja wa Urais pamoja na Makamu wake.
Taarifa za kiuchunguzi kutoka ndani ya Kambi ya Lowassa zinasema endapo Lowassa akipitishwa na Kamati kuu CC kinachofuata ni kutafuta kura za wajumbe 175 wa NEC kwa udi na Uvumba.
“Ujue sisi tunajua kabisa Lowassa akipita tu CC tayari Safari ya Matumaini imefanikiwa maana tumeshapata kura 175 za wajumbe wa NEC basi tumefanikiwa nakuhakishishi tutazipata kura hizo,tatizo ni kamati kuu ndugu,”
Jumatatu, 1 Juni 2015
NDOA ZA JINSIA MOJA ZAPATA KIBARI...SHERIA MPYA YAANZISHWA
Kinara mkuu wa chama cha upinzani cha Labour nchini Australia, ameanzisha sheria inayokubalia ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, sheria ambayo inapingwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo, Tony Abbott.
Kiongozi huyo, Bill Shorten, amemtaka Bwana Abbott kuwakubalia wanachama wa serikali wawe na uhuru wa kupiga kura kuhusiana na swala hilo.
Abbot ambaye ni mfuasi wa kanisa katoliki alikataa kura ya uhuru wa ndoa za jinsia moja na kusema kuwa lengo lake kuu ni kuimarisha uchumi na usalama wa taifa.
***chanzo na BBC Swahili***
KAZI YA KUTANGAZA NIA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) BADO INAENDELEA...NI ZAMU YA MWANDOSYA MBEYA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Kazi Maalum), Profesa Mark Mwandosya, anatarajia kutangaza nia ya kugombea urais leo Juni Mosi na kuchukua fomu Juni tatu mwaka huu.
Ijumaa, 3 Aprili 2015
PICHA ZAIDI ZA AJALI YA MASHABIKI WA SIMBA
Very sad kwa ndugu jamaa na marafiki na wapenzi wa soko nchini
Jumatano, 25 Februari 2015
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JANA KATIKA MJI MDOGO WA ILULA NJE KIDOGO YA MJI WA IRINGA
WANANCHI WALIAMUA KUCHOMA KITUO CHA POLISI NA KUZIBA BARABARA KUU YA IRINGA-DSM KWA KUCHUKIZWA NA POLISI KUMUUA MAMA MMOJA MFANYABIASHARA KATIKA MJI HUO!
Alhamisi, 22 Januari 2015
ROSE MUHANDO JELA MIAKA SABA KWA TUHUMA ZA KUTOA MIMBA YA MIEZI SABA.
Rose Muhando.
KITENDO cha
mwimbaji nyota wa muziki wa Injili, Rose Muhando (pichani) kudaiwa
kutoa mimba ya miezi saba, endapo kitathibitishwa na mamlaka
zinazohusika, kinaweza kusababisha kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 7
jela, Risasi Jumatano lina mkanda kamili.
Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili, Rose Muhando akiimba wakati akiwa mjamzito.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, ilidaiwa kuwa Rose, mwimbaji mwenye maskani
yake mjini Dodoma, alikuwa ameitoa mimba aliyokuwa nayo, ambayo
anadaiwa kupewa na mcheza shoo wake. Kama ingeenda salama na kujifungua,
ingempatia mtoto wake wa nne.
Kufuatia madai hayo,
gazeti hili lilifanya mawasiliano na wadau kadhaa, miongoni mwao wakiwa
ni wanasheria, wanamuziki wenzake na viongozi juu ya ishu hiyo
iliyoushtua ulimwengu wa Injili.
Mwanasheria mmoja maarufu
nchini, ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa sababu alizodai ni za
kimaslahi, alisema kutoa mimba ni kosa kisheria na wahusika, akiwemo
mama na daktari aliyeshiriki kukamilisha tukio hilo, wanapaswa
kushtakiwa na kuhukumiwa.
“Inategemea, kama alitoa mimba kwa sababu za kimatibabu, yaani ili afya
yake iwe sawa ni lazima atoe ujauzito alionao, hilo siyo kosa, lakini
kama alitoa kwa sababu nyinginezo nje ya hapo, ni kosa la jinai
linalostahili adhabu.
“Kwa mujibu wa Sheria za Kanuni ya Adhabu sura ya 16, kifungu cha 150,
daktari anayehusika na kosa hilo adhabu yake ni kifungo cha miaka 14
jela na mama aliyetolewa ujauzito huo, kwa mujibu wa kifungu cha 151,
anastahili kifungo cha miaka saba jela,” alisema mwanasheria huyo.
Kuhusu sababu za kumfunga kwa miaka mingi daktari badala ya mama
aliyetaka kutolewa, ‘lawyer’ huyo alisema hii inatokana na kiapo ambacho
madaktari huapa ambacho kinawataka kulinda uhai wa mtu na pia ni
kukiuka maadili ya kazi yao.
“Mahakama itakuwa kali
zaidi kwa madaktari kwa sababu ya dhamana ya kiapo chao. Huu unakuwa ni
mfano kwa madaktari wengine ili wasimamie maadili na viapo vyao,”
alisema mwanasheria huyo.
Katibu wa Chama Cha
waimba Injili, Stella Joel, alipoulizwa kuhusu maoni yake juu ya kadhia
hiyo, alisema chama chao hakina taarifa za tukio hilo, lakini wanaweza
kuchukua hatua kama Polisi watalifanyia kazi jambo hilo kwa vile ni kosa
la kijinai.
“Kutoa mimba ni kosa la Jinai, kwa hiyo kama Polisi watalifanyia kazi,
sisi tutatoa tamko na kuchukua hatua, kwa sasa hatuna la kufanya,
tunasikia katika vyombo vya habari na mitandao, tukimuuliza anakataa,”
alisema.
Waimbaji wenzake, Bahati Bukuku na Christina Shusho walionyesha
kushangazwa na tukio hilo, wakidai limewashtua na halikutarajiwa.
“Rose ni mtu mzima, kama
kweli tukio hili lipo, basi huo ni uamuzi wake na Mungu wake, inategemea
na mapatano yao, kila mtu ana maamuzi yake ila nimeshtushwa sana,”
alisema Bahati Bukuku.
Shusho alisema jambo hilo ni baya na kosa kisheria, lakini hata hivyo ni suala binafsi linalomhusu mhusika.
Rose Mhando mwenyewe
alitafutwa katika simu yake ya mkononi ili kusikia kauli yake juu ya
suala hilo, lakini zaidi ya mara nne, simu yake iliita hadi kukatika
pasipo kupokelewa.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)