Jumatatu, 16 Septemba 2013

YANGA WAMEKATA RUFAA MECHI YAO DHIDI YA MBEYA CITY



Kabla ya mchezo huo kuanza kulitokea vurugu za mashabiki baada ya mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Mbeya City kulipiga mawe basi la Yanga wakati linaingia uwanjani pamoja na gari dogo aina ya Noah lililokuwa limebeba viongozi wa Yanga nalo lilipigwa mawe na kioo cha nyuma cha gari kuvunjika.
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wamekata rufaa kwa kamati ya Ligi kutaka mchezo wao dhidi ya Mbeya City uliofanyika Jumamosi iliyopita urudiwe kwenye uwanja huru.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine ulimalizika kwa sare ya 1-1 na kufanikiwa kuingiza Sh100 milioni baada ya mashabiki 20,000 kushuhudia mechi hiyo.
Kabla ya mchezo huo kuanza kulitokea vurugu za mashabiki baada ya mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Mbeya City kulipiga mawe basi la Yanga wakati linaingia uwanjani pamoja na gari dogo aina ya Noah lililokuwa limebeba viongozi wa Yanga nalo lilipigwa mawe na kioo cha nyuma cha gari kuvunjika.
Wakizungumza jijini Mbeya, Ofisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto akisaidiana na mjumbe wa kamati ya sekretarieti ya Yanga, Patrick Naggi walisema, “Tunachohitaji mechi irudiwe na ichezwe kwenye uwanja huru.”

MADAWA YA KULEVYA YAWA GUMZO NCHINI TANZANIA

Wanigeria waliotimuliwa Kenya kwa kujihusisha na dawa za kulevya watumia Uwanja wa Ndege Dar kurejea tena. Mmoja adakwa na pakiti 400 za heroin baada ya kusafiri kwa gari  kupitia Namanga
Raia wa Nigeria aliyefukuzwa Kenya miezi minne iliyopita kwa kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya, amekamatwa tena nchini humo akiwa na pakiti 425 za heroin, akiaminika kwamba alipitia Tanzania.
Mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Enobemhe Emmanuel Peter inaaminika alishukia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akitokea Nigeria na kisha kwenda Kenya kwa barabara, kupitia mpaka wa Namanga mkoani Arusha.
Peter alikamatwa pamoja na mwanamke ambaye ni

Mdhalilishaji aliyejidai kuwa Justin Bieber



Hunter alijidai kuwa Justin Bieber ili watoto wamtumie kanda za video za ngono
Rober Hunter aliwahidi watoto kuwa angekuwa na uhusiano wa kimapenzi nao  
Mwanamume mmoja nchini katika kitongoji cha Middlesbrough, Uingereza aliyejidai kuwa mwanamuziki maarufu duniani , Justin Bieber, ili kuwahadaa watoto kuweza kumtumia kanda za video wakiwa wanafanya vitendo vya ngono, amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.
Robert Hunter, mwenye umri wa miaka 35, na ambaye alijidai kuwa 'Justin Bieber Hunter 'alikamatwa baada ya msichana mmoja kutoka Tasmania kufahamisha polisi kumhusu.
Polisi walimkamata nyumbani kwake akiwa na