Jumatano, 11 Septemba 2013

MFUMUKO WA BEI YA MAZAO WASHUKA


Hayo yalisemwa jana na Kwesigabo akizitaja bidhaa za vyakula zilizochangiwa kupungua kwa mfumuko wa bei na kiwango cha punguzo kwa asilimia katika mabano kuwa ni pamoja na mikate na nafaka (2.2), vitafunwa (3.8), mahindi ( 1.6), unga wa ngano (2.5), unga wa muhogo ( 0.6) na unga wa mtama (3.4).
Mfumuko wa bei nchini umezidi kupungua na sasa umefikia asilimia 6.7 kwa mwezi Agosti, 2013, kutoka asilimia 7.5, Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) imebainisha, katika taarifa yake ya matokeo ya mfumuko wa bei kwa mwezi Agosti.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa NBS, Ephrahim Kwesigabo alisema kupungua kwa mfumko huo wa bei kunamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Agosti imepungua kulinganisha na mwezi Julai.
“Kwa kiasi kikubwa kupungua kwa mfumuko wa bei nchini kumechangiwa na kupungua kwa

Roy Hodgson atetea England


 
 England ilienda sare tasa na Ukrain matokeo ambayo yamewakera wengi

Meneja wa timu ya Uingereza Roy Hodgson, amesema aliridhika na walivyocheza wachezaji wake walipojitosa katika michuano ya kuwania kombe la dunia.
England ilienda ilimaliza mchezo kwa sare tasa dhidi ya Ukraine kwenye mechi iliyochezwa mjini Kiev
Kikosi cha Hodgson kinasalia juu katika kikundi cha H na kitafuzu ikiwa kitashinda mechi zao mbili za kufuzu dhidi ya Montenegro na Poland zitakazochezwa katiika uwanja wa Wembley.
Baadhi ya mechi ambayo walisema ilikosa msisimuko na ambayo ilichezwa mbela ya mashabiki 70,000, meneja huyo wa England alisema, "kabla ya mchezo, hisia waliyokuwa nayo wengi ni kwamba matokeo ya sare yoyote hayatakuwa mabaya.''
England iliingia kwenye mchezo huo, bila ya wachezaji, Danny Welbeck ambaye huchezea Man U , Wayne Rooney na mshambulizi wa Liverpool Daniel Sturridge ambao hawakucheza kutokana na majeraha.
Uwezo wetu wa kushambulia ulikuwa mdogo sana kwa sababu hatukuwa na wachezaji, Rooney, Welbeck na Sturridge, alisema Hodgson.
"pia tulimpoteza kiungo cha kati, Alex Oxlade-Chamberlain kwa sababu ya jeraha la goti ingawa wachezaji waliowakilisha kwenye mchezo huo walicheza vyema.
Sare hiyo iliisongesha England mbele kwa pointi moja kwenye kundi la H ikisalia na michuano miwili.

Makao ya ujasusi yashambuliwa Misri


Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka nje ya makao makuu ya ujasusi na kuwaua watu wanne
 
Ulinzi mkali katika mpaka wa Sinai

Duru zinasema kuwa watu wanne wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo karibu na eneo la Rafah, kwenye mpaka wa Misri na ukanda wa Gaza.
Mlipuko wa pili ulilenga kuzuizi cha jeshi. Haijulikani ikiwa mtu yeyote alijeruhiwa.
Eneo la Sinai limekumbwa na mashambulizi mengi yanayofanywa na wapiganaji wa kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani rais Mohammed Morsi mapema mwezi Julai.
Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliendesha gari kwa kasi sana na