Jumatano, 11 Septemba 2013

Makao ya ujasusi yashambuliwa Misri


Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka nje ya makao makuu ya ujasusi na kuwaua watu wanne
 
Ulinzi mkali katika mpaka wa Sinai

Duru zinasema kuwa watu wanne wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo karibu na eneo la Rafah, kwenye mpaka wa Misri na ukanda wa Gaza.
Mlipuko wa pili ulilenga kuzuizi cha jeshi. Haijulikani ikiwa mtu yeyote alijeruhiwa.
Eneo la Sinai limekumbwa na mashambulizi mengi yanayofanywa na wapiganaji wa kiisilamu tangu jeshi kumwondoa mamlakani rais Mohammed Morsi mapema mwezi Julai.
Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliendesha gari kwa kasi sana na
kugonga jengo hilo. Liliporomoka huku baadhi ya wanajeshi wakikwama chini ya vifusi, kwa mujibu wa shirika la habari la AP.
Walioshuhudia shambulio hilo wanasema kuwa mlipuko mkubwa uliharibu madirisha ya jengo hilo katika eneo la Imam Ali mjini Rafah.
Punde baadaye, wanamgambo walilenga kizuizi cha jeshi barabarani kwa kuwafyatulia maguruneti.

Msako wa jeshi

Mashambulizi hayo yametokea siku chache baada ya angalau wapiganaji tisa kuuawa katika operesheni kubwa ya kijeshi, karibu na miji ya Rafah na Sheikh Zuweyid.
Mnamo tarehe 7 Septemba, helikopta za jeshi zilifanya mashambulizi ya angani, yaliyonuia kuharibu silaha , magari na maficho ya wapiganaji, katika kile kilichosemekana kuwa operesheni kubwa zaidi ya kijeshi kuwahi kushuhudiwa katika eneo hilo.
Jeshi limetuhumu bwana Morsi kwa kuwa mpole sana kwa harakati za wapiganaji, baada ya kuwaachilia wafungwa waliohusika katika harakati za makundi ya wapiganaji wa kiisilamu.

Hakuna maoni: