Ijumaa, 25 Oktoba 2013

MATUKIO KATIKA PICHA

WAZIRI MKUU MH. MIZENGO PINGA AKIPOKEA SANAMU YA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA HAINAN KUTOKA KWA M/KITI WA CHINA WA SHIRIKA HILO CHEN FENG YALIYOFANYIKA HUKO MJINI GUANGZHOU CHINA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JAKAYA KIKWETE (KULIA) AKIPEWA TAARIFA FUPI KUTOKA KWA KARANI WA MIKUTANO YA BUNGE MH. THOMAS KASHILILA ALIPOTEMBELEA MDAHALO WA BUNGE MJINI DODOMA
WASAMARIA WEMA WAKIWA WAMEMBEBA MFANYABIASHARA WA JIJI LA DSM NDG GELAS URASSA ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI NA KUPATA AJALI NA KUPELEKEA MGUU WAKE WA KULIA KUVUNJIKA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JAKAYA KIKWETE AKIONGESHA KWENYE KILELE CHA MWINUKO WA KILIMA LIGANGA SEHEMU AMBAYO KAMPUNI MOJA KUTOKA CHINA ITACHIMBA MABILION YA MAKAA YA MAWE NA MADINI YA CHUMA KWA KIPINDI CHA MIAKA 100 IJAYO.
MRADI HUO UANAPATIKANA WILAYA YA LUDEWA MKOA WA NJOMBE NA KUWANUFAISHA WAAJILIWA ZAIDI YA 32 ELFU.
MH. MZENGO PINDA WAZIRI MKUU WA TANZANIA AKIKAGUA MRADI WA UMWAGILIAJI DUJIANGYAN HUKO CHENGDU  KATIKA ZIARA YA KIMATAIFA NCHINI CHINA

Endelea kuwa nami katika blog ya kijamii na matukio.........!

WANANCHI WA MADAGASCAR HAWAKUNGOJA KUAMBIWA...WAJITOKEZA KUCHAGUA KILICHO BORA

 
Harakati za kampeni kabla ya uchaguzi wa Rais Madagascar
Wananchi wa Madagascar wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa kwanza kufanyika nchini humo tangu yalipofanyika mapinduzi yaliyoungwa mkono na jeshi miaka minne iliyopita.
Wagombea 33 wanawania urais wa nchi hiyo katika uchaguzi huo, ambao umeahirishwa mara tatu mwaka huu.
Wagombea wawili wanaopewa nafasi ya kushinda, wanaahidi kujenga upya uchumi wa Madagascar baada ya miaka ya mgogoro wa kisiasa na kiuchumi.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, zaidi ya asilimia 92% ya wananchi milioni 21 wa Madagascar wanaishi chini ya dola mbili kwa siku.
Rais Andry Rajoelina alimng'oa madarakani Marc Ravalomanana mwaka 2009, na kulitumbukiza taifa hilo katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kusababisha nchi hiyo kutengwa na jumuiya ya kimataifa na kunyimwa misaada kutoka nje.
 MVUTANO WA KISIASA
Baada ya kupora madaraka, Bwana Rajoelina alitangaza kuwa kungekuwa na katiba mpya na uchaguzi kufanyika ndani ya miezi 24.
Mwezi Mei mwaka 2009 ilikubalika kuwa marais wote wa zamani wangeruhusiwa kugombea katika uchaguzi. Hata hivyo hilo halikufanyika mwaka 2009 au 2010.
WAGOMBEA URAIS WALIOENGULIWA KWENYE KINYANG'ANYIRO
Mwezi Januari mwaka huu Bwana Rajoelina na Bwana Ravalomanana wote walikubali kutogombea katika uchaguzi huu, ikiwa ni makubaliano na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, chombo cha kikanda ambacho Madagascar ni moja ya nchi wanachama wake.
Awamu ya kwanza ya uchaguzi huu, ulipangwa kufanyika Julai 2013 lakini ukasogezwa mbele hadi mwezi Agosti kwa sababu mke wa Bwana Ravalomanana, Lalao - na baadaye Bwana Rajoelina mwenyewe kuamua kugombea, hali iliyosababisha nchi wahisani kusitisha fedha kwa ajili ya uchaguzi huo.
Bwana Rajoelina na Lalao Ravalomanana walizuiwa kugombea na mahakama ya uchaguzi pia ilimwondoa katika orodha ya wagombea, rais wa zamani Didier Ratsiraka baada ya wote watatu kukataa kujiondoa.