Shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) linasema
kuwa angalau watu 800,000 wametoroka makwao kufuatia vita kati ya
serikali na waasi wa M23. Kundi hilo lilianza harakati zake dhidi ya
serikali mwezi Aprili mwaka 2012.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, inasema kuwa wanajeshi wake wamekomboa
ngome mbili za mwisho za waasi wa M23, Tshangu na Runyoni mapema
Jumanne.
Waasi wa M23 walitoroka maeneo waliyokuwa wameyateka ya sehemu za
milimani nchini DRC baada ya jeshi la serikali kukataa ombi la kusitisha
vita ili kufanya mazungumzo na serikali na hata kuwaondoa kutoka katika
maeneo waliyokuwa wameyadhibiti.
Jeshi la Congo liliungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuwapiga waasi wa M23 Mashariki mwa DRC.
Rutshuru ni moja ya maeneo yaliyokombolewa na jeshi la serikali ya DRC, tangu mwishoni mwa wiki
Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini ni maeneo yenye utajiri mkubwa wa
madini na yamekuwa kitovu cha mgogoro wa kisiasa ambao umekuwa
ukitokota DRC kwa miaka mingi.
ENDELEA KUWA NASI KWA MATUKIO ZAIDI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni