Jumanne, 17 Desemba 2013

MANGARIBA 38 WAKAMATWA HUKO MOSHI MKOANI KILIMANJARO

 
Ukeketaji hufanywa katika sehemu nyingi Tanzania licha ya kuharamishwa
Maafisa wakuu mjini Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wamewakamata wanawake 38 waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.
Haijulikani idadi ya wasichana waliokuwa wanakeketwa , lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.
Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini hapa nchini , hilo sio jambo la kawaida mjini Moshi.
Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa Jumapili walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.
Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.
Ukeketaji umeharamishwa hapa nchini tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu mabalimbali za nchi.
Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa hapa nchini.

Hakuna maoni: