Ijumaa, 27 Septemba 2013

KWA UFUPI

KENYA YAMSAKA SAMANTHA LEWTHWAITE

Polisi wa kimataifa Interpol, wamemuweka mwanamke aliyeshukiwa kuongoza mashabulizi ya kigaidi nchini Kenya raia Muingereza Samantha Lewthwaite, kwenye orodha ya watu wanaosakwa
 sana duniani.

UN YAJADILI AZIMIO KUHUSU SYRIA
 
 Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linajadili rasimu ya azimio kuhusu silaha za kemikali za Syria baada ya Marekani na Urusi kukubali mapendekezo ya azimio hilo.

AFUNGWA MIEZI SITA JELA KWA WIMBO WA MATUSI TUNISIA
 
Msanii wa kizazi kipya nchini Tunisia, Ahmed Ben Ahmed, anayejulikana kwa jina la kiusanii, Klay BBJ, amehukumiwa jela kwa miezi sita kwa kuwatusi maafisa wakuu kupitia kwa  
muziki wake.

Hakuna maoni: