Jumatatu, 4 Novemba 2013

KUFAIL MTIHANI SIYO KUFAIL MAISHA...ONA JINSI MWANAFUNZI ALIVYOJINYONGA HADI KUFA KUOGOPA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE

 
Mwanafunzi aliyekuwa akisoma  shule  ya  sekondari  Sabasaba  mjini  Iringa akijiandaa kurudia  kufanya  mtihani  wa  taifa  wa kidato  cha nne kupitia  kituo  cha Krelluu mjini  Iringa Khamis Mkundo  mkazi  wa Mwangata  C katika manispaa ya  Iringa amejiua kwa kujinyonga  kwa kamba kwa kile  alichodai  kuchoshwa na kufeli  mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.

Katika  barua  yake  ndefu aliyoiandika  kijana  huyo amesema  kuwa amefanya  hivyo si kwa kujipendea  ila amechukizwa na hatua yake ya  kufeli mara kwa mara  hivyo  kuamua  kujiua ili  kuepuka aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.

Shemeji  wa  kijana  huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao  matukiodaima.com  kuwa  tukio  hilo limetokea mida ya saa 12 na saa 1  usiku wa  leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda  mrefu  kwa kijana  huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi  mtihani  wa kidato cha nne  bila mafanikio.

Kijana huyo  alisema hajapenda  kuona anaendelea  kufeli na kuwa  yupo tayari kwa lolote  kukwepa aibu ambayo ipo mbele  yake.
 
Hata  hivyo kufuatia mazungumzo hayo, kijana huyo aliagana na ndugu zake akiwemo kaka  yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani  hapo kabla  ya kijana  huyo kukutwa amejinyonga.

Mwenyekiti  wa serikali  ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha  kutokea kwa kifo  hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana  huyo ameuacha .
 
 
 
 
HII NI BARUA ALIYOIANDIKA KABLA HAJAJINYONGA AKIWATAJA BAADHI YA 

MARAFIKI NA WAZAZI WAKE AKIWATAKIA MAISHA MEMA 

CHANZO..Matukio Daima.com

Hakuna maoni: