
Mlipuko mkubwa umetokea katika mji wa Mogadishu nchini Somali karibu na uwanja wa ndege.
Duru zimearifu kuwa mlipuko huo huenda umesababishwa na mtu aliyejitolea muhanga aliyejilipua ndani ya gari.
Kundi
la wapiganaji wa kiislamu la Al- Shaabab mara kwa mara hutumia milipuko
ya magari, lakini kufikia sasa halijakiri kuhusika na mlipuko huo.
Haijajulikana ni watu wangapi wameuwawa.
CHANZO NA: BBC SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni