Maafisa wa utawala nchini
Nigeria wanasema kuwa hapakuwa na ulinzi katika chuo cha mafunzo ya
kilimo nchini Nigeria ambako hadi wanafunzi 50 waliuawa Jumapili.
Wanafunzi waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa
wapiganaji wa kiisilamu katika mabweni yao katika jimbo la Yobe ,
Kaskzini Mashariki mwa Nigeria.
Afisaa mmoja aliambia BBC kuwa serikali itashirikiana na jeshi kuhakikisha kuna ulinzi katika shule.
Serikali ya Nigeria ilisema kuwa haitafunga
shule zingine kutokana na shambulio lililowaua wanafunzi 50 katika chuo
kikuu cha mafunzo ya kilimo.
Shambulio hilo linashukiwa kufanywa na
wanamgambo wa Boko Haram siku ya Jumapili.Wavamizi walishambulia kwa
risasi chuo hicho kilichoko jimbo la Yobe, kaskazini mashariki mwa
Nigeria.
Afisa mmoja wa serikali Abdullahi Bego, ameambia
BBC kuwa serikali na idara ya jeshi zitaongeza usalama katika taasisi
zote za elimu.
Eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria
limewekwa katika hali ya hatari kufuatia mashambulio yanayofanywa kila
mara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Boko Haram wanadaiwa kupigana kwa lengo la
kuiondoa serikali iliyoko na badala yake kuweka utawala wa kiislamu.
Tayari wamefanya mashambulio kadhaa katika shule.
Vyombo vya usalama
Mwandishi wa BBC wa idhaa ya Hausa, Mansur
Liman, anasema kuwa huenda jeshi la Nigeria imelegeza juhudi zake
kufuatia kufanikiwa kwao katika siku za hivi punde kuwaondosha
wapiganaji wa Boko Haram kutoka maeneo mengi kaskazini mashariki.
Hata hivyo wapiganaji hao wameripotiwa kuiba
sare za kijeshi katika siku kadhaa zilizopita na magari ya kivita.
Inadaiwa wanatumia vifaa hivi kupenya maeneo yaliyowekwa ulinzi mkali.
Mshauri mkuu wa serikali katika Jimbo la Yobe,
Abdillahi Bego, ameambia BBC, Jumatatu, kuwa hakukuwepo walinzi katika
eneo hilo wakati shambulio lilifanywa katika chuo kikuu.
Amesema kuwa maafisa wa usalama wa Nigeria walistahili kuimarisha doria katika taasisi za elimu zote.
Amesisitiza kuwa shule zingine hazitafungwa kwani hilo ndilo hao ''magaidi'' wanataka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni