
Katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, siku hiyo ya Jumanne mtoto akitembea na bunduki bandia kwenye ufuo wa bahari ya Lido

Mnamo siku ya Jumapili, kijana huyu anaonekana akicheza na mpira katika
kambi ya watu walioachwa bila makao kufuatia mapigano katika mkoa wa
Kivu Kaskazini karibu na mji wa Goma

Siku mbili baadaye mama huyu anaanda Ugali katika mji katika kambi nyingine karibu na mji wa Goma

Mwanamume mmoja Mashariki mwa mji wa Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria anapuliza ala yake ya muziki wakati wa sherehe za Idd

Mji wa Maiduguri ni kitovu cha harakati za Boko Haram na hii ndio mara
ya kwanza kwa sherehe za idd kufanyika mjini humo tangu kundi hilo
kuanza harakati zake

Mwanamke anawaelekeza vipofu watatu ambao huimba wakati wakiomba pesa katika soko moja mjini Bamako, Mali

Familia ambazo nyumba zao ziliharibiwa kwenye mafuriko mjini, Khartoum,
wanapumuzika kwenye vitanda vyao kando ya barabara Jumanne. Mashirika ya
misaada yalisema kuwa watu 11 walifariki na wengine 98,500 wameathiriwa
na mafuriko hayo ambayo chanzo chake ni mvua kubwa ambayo imekuwa
ikinyesha tangu tarehe moja hadi nne mwezi huu

Mashua ya uvuvi kwenye ufuo wa bahari katika mji mkuu wa Senegal , Dakar
ikielekea baharini siku ya Jumanne ambako boti moja iliharibika na
kuvuja mafuta. Hali ingali kudhibitiwa na tayari imezua wasiwasi kuhusu
uharibifiu wa mazingira
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni