Visima vikubwa vimegunduliwa chini ya ardhi katika eneo kame la Turkana
Kaskazini mwa Kenya . Hii ni kwa mujibu wa tangazo la serikali ya nchi
hiyo.
Serikali
inakadiria kuwa visima hivyo vilivyopatikana kwa kutumia picha za
satelite , huenda vikakidhi mahitaji ya maji kwa nchi nzima kwa kipindi
cha miaka sabini.
Watu wa jamii ya Turkana ni watu wa kuhamahama na huathirika mno wakati
wa ukosefu wa mvua kwani ina maana kuwa wanakosa maji kwa mifugo wao.
Ugunduzi huo wa maji ulitangazwa wakati wa ufunguzi wa kongamano la
kimataifa kuhusu maji nchini Kenya
lililoandaliwa na shirika la Unesco. Shirika hilo lilishirikiana na
serikali ya Kenya pamoja na shirika la maendeleo la Japan JICA
Waziri
alisema kuwa kipaombele kinapewa mwanzo kukidhi mahitaji ya watu wa
eneo hilo. ''Tunatarajia kuwa maji yataweza kupatikana katika kipindi
cha mwezi mmoja ujao,'' alisema waziri .
Maji hayo pia yatatumiwa kwa kilimo cha unyunyiziaji na viwanda. Hivi
maajuzi mafuta yaligunduliwa Turkana na kulifanya eneo hili kuonekana
kuwa na utajiri wa rasilimali.
Licha ya rasilimali hizi, wakaazi wa eneo hili wanaishi katika umaskini
mkubwa mbali na kuhisi kuwa wametengwa .Wanatarajia kuwa serikali
itaweza kuwashirikisha katika uamuzi wa ambavyo rasilimali hizi zinaweza
kutumika ili kuwafaidi wakaazi
Wanaharakati wanataka serikali ielewe umuhimu wa kushirikisha wakaazi na
kuwapa fursa wao wenyewe kusema ambavyo wanataka rasilimali zao
zitumike
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni