Maafisa wa usalama nchini Sudan
wamewaua watu 50 katika maandamano yaliyofanywa kwa siku kadhaa kupinga
hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta. Taarifa hii ni kwa mujibu wa
mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo.
Polisi waliwatupia gesi ya kutoa machozi waandamanaji zaidi siku ya Ijumaa.
Maafisa wanasema kuwa chini ya watu 29
wamefariki na kusema kuwa serikali ilikuwa haiwezi tena kumudu gharama
ya ruzuku ya mafuta.
Waandamanaji wameikosoa serikali ya Rais Omar al-Bashir kwa hatua hii na kumtaka aondoke mamlakani.
Taasisi ya elimu ya maswala ya haki na amani
pamoja na shirika la Amnesty International zimesema kuwa watu wamepata
majeraha ya risasi kwenye vifua na vichwa kulingana na jamaa, madaktari
na waandishi wa habari.
Kijana mwenye umri wa miaka 14 alikuwa miongoni
mwa waathiriwa wengi waliokuwa kati ya umri wa miaka 19-26. Waliongeza
kusema kuwa mamia ya watu wamezuiliwa.
"Kuwaua kwa kuwapiga risasi watu kwenye vifua na
vichwani ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na Sudan lazima
isitishe ghasia hizi mara moja,’’ alisema Lucy Freeman, Naibu mkurugenzi
wa shirika la Amnesty International.
Duru za hospitalini zimeambia BBC kuwa takriban watu 60 wameuawa.
Maafis wa serikali ya Sudan bado hawajasema
chochote kuhusu mauaji hayo lakini waziri wa habari Ahmed Belal Osman
alisema kuwa idadi ya vifo ambayo ni juu zaidi ya watu 29 sio sawa.
Ghasia zilianza Jumatatu pale serikali
ilipoondoa ruzuku kwa mafuta ili kupandisha ushuru. Hatua ya serikali
kupunguza gharama ya matumizi ya pesa za umma, ilisababisha kupanda kwa
bei ya mafuta na kuwaathiri sana watu wa kipato cha chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni