Jumapili, 15 Septemba 2013

Obama awasiliana na rais mpya wa Iran

Obama akizungumza juu ya Iran
Rais wa Marekani Barack Obama 
Rais Obama anasema ameandikiana barua na rais mpya wa Iran, Hasan Rouhani.
Akihojiwa na televisheni ya Marekani, ABC, Bwana Obama alisema Iran inafahamu kuwa sera ya Iran ya kujaribu kuunda silaha za nuklia ni swala kubwa zaidi kwa Marekani kushinda silaha za kemikali zilizotumiwa na Syria.
Rais Obama ametokeza mara nyingi kwenye televisheni za Marekani katika wiki za karibuni kuwakumbusha watu tishio la silaha za kemikali za Syria.
Jumapili aliulizwa jee Iran itafikiria vipi msuko-suko wa Syria?.
Rais Obama alisema amewasiliana na rais mpya wa Iran, Bwana Rouhani.
Na alisema kuna tofauti baina ya Iran na Syria.
Alikiri kuwa mradi wa nuklia wa Iran unavotishia Israil, ni jambo lilo karibu na masilahi ya Marekani kushinda silaha za kemikali.
Aliongeza kusema kuwa mashindano ya kumiliki silaha za nuklia yanaweza kutibua sana eneo hilo.
Akilinganisha Iran na Syria, Rais Obama alisema anafikiri Iran inatambua kwamba kuna njia ya kusuluhisha maswala haya kidiplomasia, ingawa alikiri kuwa ni vigumu kuzungumza na Iran.


Hakuna maoni: