ASKALI AKIWA MAKINI KULINDA AMANI KENYA
VIKOSI VYA UOKOAJI VIKIOKOA MAJERUHI HAPO KENYA
RAIA WA KENYA WAKIWA HAWAAMINI KILICHOWAKUTA
Taharuki ilianza saa saba mchana Jumamosi baada ya watu wanaokisiwa kuwa
kumi kuvamia duka kubwa la Nakumat ndani ya jengo la kifahari la
Westgate
Baadhi walifanikiwa kunusurika kifo kwa usaidizi wa polisi waliofika mara moja kuanza kukabiliana na washambuliaji
Hali ya usalama imeweza kudhibitiwa , eneo lililoshambuliwa limezingirwa na wanajeshi wakisaidiwa na polisi na watu wlaifika kuwatafuta jamaa zao wamezuiwa.
Polisi waliweza kufika mara moja katika eneo la shambulio kukabiliana na wapiganaji ambao idadi yao kamili haijaweza kusemwa
Polisi wakiwa katika harakati za kuwaokoa baadhi ya wakenya waliokuwemo ndani ya jengo hilo
Washambuliaji wa kundi la kigaidi la Al Shabaab walivamia jengo hilo na kuwapiga risasi kiholela watu waliokuwemo
Baadhi ya manusura waliofanikiwa kuokolewa kutoka katika jengo la Westgate
Kikosi cha wanajeshi wa KDF wanasema kuwa wanafanya kila hali kuhakikisha kuwa wanamgambo walio ndani ya jengo hilo hatimaye wattaweza kukamatwa
Hali ilikuwa mbaya kwani washambuliaji waliwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa ndani ya jengo hilo na hawa wanaonekana kukimbilia usalama wao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni