Mtoto wa miaka minne ambaye ni raia wa Uingereza, Elliott Prior ameonyesha ushujaa wa hali ya juu baada ya kuweza kuwatolea maneno makali na ya kugusa magaidi waliovamia jengo la maduka la Westgate.
Mama huyo anasema baada ya kuwaachia walimshawishi yeye na
watoto wake kujiunga na dini ya Kiislamu wakidai kuwa, imani ya dini ya
Kiisilamu haina ubaya wowote.
“Aliniambia natakiwa kubadili dini niwe Muislamu,
na akaniuliza ‘unatusamehe, unatusamehe)” mama huyo aliliambia gazeti
la Independent la Uingereza.
“Kwa kawaida ningesema tu chochote walichotaka ili watuachie tuondoke,” anasema mama huyo.
Baadaye magaidi hao waliwaruhusu watoto hao kutoka
nje ya jengo hilo wakiwa na watoto wengine wawili akiwamo mmoja mwenye
umri wa miaka 12 ambaye awali alikuwa akikataa kutoka, aking’ang’ania
kwenye mwili wa mama yake ambaye alikuwa ameshafariki.
Mama wa mtoto Elliott anasema kuwa, walifanikiwa kutoka kwenye mikono ya magaidi hao kimiujiza.
Anasema kuwa, pamoja na vitu vingine walifika kwenye duka hilo ili wakanunue maziwa.
Amber anasema kuwa, magaidi hao waliwaeleza kuwa lengo lao ni kutaka kuwaua raia wa Kenya na wale wa Marekani tu.
Baadaye watoto hao walikuja kuonekana nje ya jengo
hilo wakiwa wameshikilia chokleti ambazo wanadaiwa kupewa na magaidi
hao, huku pembeni yao kukiwa na mwili wa mtu aliyefariki dunia.
Baba wa mtoto huyo, anasema kupona kwa familia
yake kwenye tukio hilo ambalo magaidi hao waliua zaidi ya watu 62, ni
muujiza wa aina yake.
“Nashukuru sana familia yangu iko salama,
nilidhani watakuwa miongoni mwa wale ambao hawakuwa na bahati,’’ Prior
alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari.
‘‘Kwa sasa kama familia tunataka muda kidogo na
faragha, lakini tunaomba sana wale wanaotaka kusaidia majeruhi wa tukio
hili huko Kenya, watoe msaada wao kupitia Shirika la Msalaba Mwekundu
Kenya,”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni