Haya ni miongoni mwa mashambulizi makubwa ya kigaidi ambayo yamewahi kutekelezwa katika kanda ya Afrika Mashariki.
Septemba. 21, 2013: Magaidi
walitumia maguruneti na bunduki kushambulia jengo la kifahari la
Westgate mjini Nairobi, Kenya lenye maduka na mikahawa themanini na
kuwaua watu zaidi ya sitini huku zaidi ya 175 wakijeruhiwa.Kundi la
kigaidi la Al-Shabab lilikiri kufanya shambulizi hilo.
Oktoba 2011-Machi 2013: Al
Shabaab na wapiganaji wake walifanya mashambilizi kadhaa nchini Kenya na
kuwaua zaidi ya watu sitini wakilipiza kisasi kile walichosema ni hatua
ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini huo kupigana dhidi yao. Serikali
ya Kenya ilituma vikosi vyake nchini Somalia baada ya al-Shabab kufanya
mashambulizi kadhaa katika maeneo ya mipakani pamoja na kuwateka nyara
watalii wa kigeni.
Mnamo mwezi Julai tarehe 11,mwaka 2010:
Wanamgambo wa Al Shabaab walilipua misururu ya mabomu katika mji mkuu
wa Uganda Kampala, katika mkahawa ambako mashabiki wa soka walikuwa
wanatizama fainali ya michuano ya kombe la dunia, kwenye skrini kubwa.
Takriban watu 76 waliuawa. Kundi la Al-Shabab lilisema kuwa mashambulizi
hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Uganda kujihusisha na vita dhidi
ya kundi hilo Somalia.
Tarehe 28 mwezi Novemba, mwaka 2002:
Kundi hilo la kigaidi lilishambulia hoteli ya kifahari iliyokuwa
inamilikiwa na waisraeli, katika eneo la Kikambala karibu na mji wa
Mombasa na kuwaua watu 13. Dakika chache kabla ya shambulii hilo,
magaidi hao waliifyatulia makombora ndege ya kiisiralei iliyokuwa
inaruka katika uwanja wa kimataifa wa Mombasa, lakini waliikosa.
Mnamo tarehe saba Agosti, 7 mwaka 1998:
Kundi lengine la kigaidi la Al-Qaida ilishambulia balozi za Marekani
mjini Nairobi na Dar es Salam. Mashambulizi hayo yaliwaua watu 224 ,
wengi wakiwa wakenya . Raia 123 wa Marekani pia waliuawa. Wengine wengi
pia walifuawa nchini Tanzaia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni