Washidani katika mashindano ya mwanadada mrembo zaidi ya Miss Jacaranda
nchini Zimbabwe wakionyesha hapa viatu vyao tayari kwa kutembea kwa
madaha ukumbini
Mjini Moscow Miss Tanzaia 2013 Betty Omara hapa anaonekana akirembwa
kabla ya kupigwa picha. Shindano la mwanamke mrembo zaidi ulimwenguni
litafanyika nchini Urusi mwezi Novemba ,9
Hapa wanamitindo wa kiume wakiwa mjini Lagos wakishiriki onyesho la mitindo
Vijana wanadansi wa Nigeria wanaojulikana kama Space Unlimited
wanashiriki mashindano ya kimataifa ya wakali wa Breakdance nchini
Ujerumani siku ya Jumamosi
Siku ya Alhamisi kijana huyu alionekana mjini Mogadishu akiwabeba Samaki
kutoka baharini katika eneo la Hamarweyne, si mavuno hayo?
Papa Francis hapa anaonekana akiongea na Chantelle Biya mke wa Rais wa
Cameroon wakati alipokutana naye mjini Vatican siku ya Ijumaa
Mwanamke huyu alikuwa nchini Tunisia na hapa anaonekana akiweka alama
ya moyo kwenye ngao ya polisi wakati wa maandamano siku ya Jumatano
mjini Tunis
Hii ni DVD yenye filamu kuhusu shambulizi la Westgate inayouzwa na
mchuuzi mjini Nairobi. Watu 67 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa
kwenye mashambulizi ya kigaidi dhidi ya jengo la Westgate mwezi jana.
Kundi la Alshabaab lilikiri kufanya shambulizi hilo.
Hawa ni wanajeshi wanawake wa Kenya wakiwa katika uwanja wa kitaifa wa
Nyayo wakati wa sherehe za kuwakumbuka mashujaa wa Kenya
Wacheza soka wa Morocco, wanasherehekea baada ya kuingiza bao katika
mechi waliyoshinda dhidi ya Croatia siku ya Ijumaa kwa mababo 3-1
Mjini Antananrivo, kijana huyu anaonekana akiuza vifagio
Katika mji huohuo, mtoto huyu alipigwa picha akiwa nyuma na ndizi zilizo
katika kibanda cha babake cha kufanyia biashara kabla ya kufanyika
uchaguzi mkuu
Watu mjini Zwedru Liberia, wanapeperusha bendera ya Ivory Coast, huku
rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara na mwenzake wa Liberia Ellen Johnson
Sirleaf wakihudhuria mkutano wa viongozi wa kijamii siku ya Jumamosi.
Liberia ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya 62,000 wa Ivory Coast
waliotoroka ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2010
USIKOSE WIKI IJAO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni