Ijumaa, 4 Oktoba 2013

MAUAJI YA BINADAMU MPAKA LINI?

MHUBIRI WA KIISLAMU AUAWA MOMBASA
 
Salim Adbi pekee ndiye aliyenusurika kifo 
 
Marehemu Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Shabaab
 
Kiongozi mmoja wa dini ya kiisilamu ameuawa kwa kupigwa risasi pamoja na watu wengine mjini Mombasa, Pwani ya Kenya.

Haijulikani aliyetekeleza mauaji hayo ya usiku wa kuamkia leo huku kukiendelea kuwa na hali ya wasiwasi miongini mwa waisilamu na maafisa wa usalama mjini humo. 


Sheikh Ibrahim Rogo alikuwa muhubiri katika msikiti alipokuwa akihubiri marehemu Sheikh Aboud Rogo ambaye pia aliuawa kwa kupigwa risasi. Aliuawa na watu wengine watatu walipokuwa wanrejea nyumbani Alhamisi usiku baada ya kuhubiri.

Sheikh Rogo alishutumiwa kutoa mafunzo yenye itikadi kali yaliyowashawishi vijana kujiunga na makundi ya kigaidi kama Alshaabab.

Mauaji haya ni sawa na ya marehemu Aboud Rogo Mohammed mwaka jana na ambayo yalisababisha ghasia mjini humo. 

Yanakuja wiki mbili tu baada ya shambulizi la kigaidi lililofanywa dhidi ya jumba la maduka la Westgate ambapo watu 67 waliuawa 

Kundi la kigaidi la al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi hayo ya kigaidi.
Aboud Rogo alidaiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Shabab na baadhi ya waisilamu walioshutumu polisi waliomuua walisema kuwa yalikuwa madai tu wala.

Ibrahim Rogo alionekana kama mrithi wa marehemu Aboud Rogo, alipohutubu katika msikiti huo.

Hakuna maoni: