
Msako umeanza mjini Paris Ufaransa, baada ya mtu aliyekuwa amejihami kushambulia ofisi za za vyombo vya habari

Mpiga picha mwenye umri wa miaka 27, alijeruhiwa vibaya katika jengo
hili la Liberation na dereva mmoja alilazimika kupitia eneo la Champs
Elysees kabla ya kuruhisiwa kupita

Polisi wanaendelea na uchunguzi wao, huku ulinzi ukiwa umedhibitiwa
katika ofisi za vyombo vya habari. Polisi wanamsaka mwanamume aliyevamia
ofisi kituo cha televisheni cha BFMTV mnamo siku ya Ijumaa.

Mshambuliaji alivamia ofisi hiyo mjini Paris na kuanza kushambulia watu kwa bunduki

Polisi sasa wako nje ya ofisi kuu za vyombo vya habari kushika doria mjini Paris

Vyombo vya habari mjini Paris vinasema kuwa mtu huyo aliyekuwa amejihami
na kumteka nyara dereva mmoja alimwambia kuwa alikuwa amejihami kwa
maguruneti

Kulikuwa na hofu kuwa mwanamume huyo alikuwa anaelekea katika jengo refuu zaidi mjini Paris la Eiffel

Watu wametakiwa kukaa majumbani mwao. Hata hivyo wanasema kuwa mshukiwa ametulia

Maafisa wakuu wakiwemo Waziri wa mambo ya ndani Manuel Valls, alizuru ofisi za Liberation baada ya shambulizi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni