Jumatatu, 9 Septemba 2013

MATUKIO KATIKA PICHA-AFRIKA

  • Mwenyeji wa mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini akifanya mazoezi yake katika moja ya kumbi za mazoezi mnamo Jumatatu , baada ya msimu wa baridi ambao uliacha eneo hilo likuwa limejaa theluji. 
     
  • Wakati mjini Mogadishu siku ya Jumanne , polisi anatoroka eneo kulikotokea mlipuko wa bomu katika kiwanda kimoja cha Petroli katika uliokuwa ubalozi wa Marekani. Marekani ilifunga ubalozi wake mjini Mogadishu zaidi ya miaka ishirini iliyopita baada ya nchi kutumbukia kwenye vita
     
  • Hapa, mwanariadha maarufu wa Ethiopia, Kenenisa Bekele, 31, anaonekana akifanya mazoezi nje ya kambi ya mazoezi mjini Addis Ababa mnamo Jumapili. Mwanariadha huyo wa mbio za masafa marefu, anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 5,000 na 10,000 anasema bado hajatafakari kuhusu kusalimu amri katika riadha anajianda kwa michezo ya olimpiki itakayofanyika Rio mwaka 2014. 
     
  • Bango hili lilitolewa siku ya Jumatatu kutangaza mchuano kati ya wanamasumbwi, Catherine Phiri Kushoto, kutoka Zambia na Toma Hawa Babirye kutoka Uganda. Mchuano utafanyika mjini Lusaka Zambia.Phiri, mwenye umri wa miaka 19 mwanafunzi wa shule anatarajiwa na wengi kushinda.
     
  • Wasichana wanasarakasi kutoka Angola wakishiriki mashindano ya kimataifa ya sarakasi nchini Urusi
     
  • Watu wanaoenakana hapa wakiokota karatasi na plastiki katika jaa la taka nchini Ivory Coast . Hutumika kwa kutengeza chupa na karatasi za plastiki
     
  • Mjini Johannesburg, mtu huyo ametoa chupa kuu kuu kwenye jaa la taka kupeleka viwandani ambako chupa nyengine mpya hutengezwa
     
  • Watoto hawa wanigeria ni mapacha ambao viungo vyao vimeshikana , hapa ni baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India 
     
  • Mwanamalkia wa Denmar Mary wakati wa ziara yake nchini Morocco

18 wauawa kwenye makabiliano na Boko Haram

Makundi ya vijana yanasaidia jeshi kutoa ulinzi kwa raia Nigeria

Takriban watu 18 wamefariki kwenye makabiliano makali kati ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram na kundi la kijamii la kutoa ulinzi kwa raia, katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wengi wa wale waliouawa waliaminika kuwa vijana wanaotoa ulinzi kwa wanavijiji waliokuwa wanatoa ulinzi kwa mji wa Benisheik dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Makabiliano hayo yametokea siku chache baada ya

William Ruto aelekea ICC kwa kesi

Naibu rais William Ruto 

Naibu rais wa Kenya William Ruto, ameondoka kuelekea Hague Uholanzi ambako anakabiliwa na kesi ya uhalifu dhidi ya binadamau katika mahakama ya ICC. Kesi yake inatarajiwa kuanza siku ya Jumanne.
Maafisa wakuu wa serikali walimuaga Ruto katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.
Bwana Ruto na rais Uhuru Kenyatta, wameshtakiwa kwa kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu, ingawa wanakana kuhusika na mauaji yaliyotokea kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008.
Mnamo siku ya Jumapili, Rais Kenyatta alisema kuwa ICC

Waliomteka nyara Askofu wasakwa Nigeria

Askofu Ignatius Kattey

Polisi nchini Nigeria wanawasaka wanaume waliomteka nyara kiongozi wa ngazi ya pili wa kanisa la kianglikana nchini Nigeria Askofu mkuu Ignatius Kattey.
Askofu Ignatius ni mkuu wa kanisa la kianglikana tawi la jimbo la Niger Delta.
Alitekwa nyara Ijumaa jioni akiwa na mkewe Beatrice, karibu na makao yao mjini Port Harcourt, Kusini mwa nchi.
Katika miaka ya hivi karibuni, visa vya watu kuteka nyara wakati wakidai kulipwa kikombozi vimekuwa jambo la kawaida katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta linalozingira Port Harcourt
Mwaka jana mamake waziri wa fedha, Ngozi Okonjo-Iweala alitekwa nyara na kuzuiliwa kwa siku tano.
Hakuna kundi lolote limedai kumkamta Askofu huyo akiwa na mkewe.
Makundi mengi ya magenge ya watu waliojihami, huendesha shughuli zao katika eneo hilo kutokana na miaka mingi ya migogoro katika eneo hilo dhidi ya sekta ya mafuta.

Wanafunzi 868,030 kuhitimu Darasa la Saba


Ni kwa nchi nzima, ambapo mwaka huu matokeo hayo ni muhimu kwa taifa kujipima kuhusu mpango wake mpya wa matokeo makubwa sasa.

Wanafunzi 868,030 wa Darasa la Saba wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi Jumatano na Alhamisi wiki hii, ikiwa ni mwanzo wa mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa utakaotekelezwa kwa kuanzia katika mitihani hiyo.
  Taarifa ya Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), inaonyesha kuwa wanafunzi hao wanatoka kwenye shule 15,677 zikiwamo za umma na binafsi.
  Inaeleza taarifa hiyo kuwa, wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mtihani wa lugha ya Kiswahili ni 844,810  kati yao wasichana wakiwa 444,475 na wavulana 400,335.    Kati ya wanafunzi hao, wasioona ni 88 wavulana wakiwa ni 56 na wasichana 32 huku