Jumatatu, 9 Septemba 2013

MATUKIO KATIKA PICHA-AFRIKA

  • Mwenyeji wa mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini akifanya mazoezi yake katika moja ya kumbi za mazoezi mnamo Jumatatu , baada ya msimu wa baridi ambao uliacha eneo hilo likuwa limejaa theluji. 
     
  • Wakati mjini Mogadishu siku ya Jumanne , polisi anatoroka eneo kulikotokea mlipuko wa bomu katika kiwanda kimoja cha Petroli katika uliokuwa ubalozi wa Marekani. Marekani ilifunga ubalozi wake mjini Mogadishu zaidi ya miaka ishirini iliyopita baada ya nchi kutumbukia kwenye vita
     
  • Hapa, mwanariadha maarufu wa Ethiopia, Kenenisa Bekele, 31, anaonekana akifanya mazoezi nje ya kambi ya mazoezi mjini Addis Ababa mnamo Jumapili. Mwanariadha huyo wa mbio za masafa marefu, anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 5,000 na 10,000 anasema bado hajatafakari kuhusu kusalimu amri katika riadha anajianda kwa michezo ya olimpiki itakayofanyika Rio mwaka 2014. 
     
  • Bango hili lilitolewa siku ya Jumatatu kutangaza mchuano kati ya wanamasumbwi, Catherine Phiri Kushoto, kutoka Zambia na Toma Hawa Babirye kutoka Uganda. Mchuano utafanyika mjini Lusaka Zambia.Phiri, mwenye umri wa miaka 19 mwanafunzi wa shule anatarajiwa na wengi kushinda.
     
  • Wasichana wanasarakasi kutoka Angola wakishiriki mashindano ya kimataifa ya sarakasi nchini Urusi
     
  • Watu wanaoenakana hapa wakiokota karatasi na plastiki katika jaa la taka nchini Ivory Coast . Hutumika kwa kutengeza chupa na karatasi za plastiki
     
  • Mjini Johannesburg, mtu huyo ametoa chupa kuu kuu kwenye jaa la taka kupeleka viwandani ambako chupa nyengine mpya hutengezwa
     
  • Watoto hawa wanigeria ni mapacha ambao viungo vyao vimeshikana , hapa ni baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India 
     
  • Mwanamalkia wa Denmar Mary wakati wa ziara yake nchini Morocco

Hakuna maoni: