Waziri mkuu wa Libya ametekwa nyara na watu wasiojulikana na ambao walikuwa wamejihami kutoka nyumbani kwake mjini Tripoli.
Duru zinasema kuwa bwana Ali Zeidan ametekwa
nyara na kupelekwa katika eneo lisilojukana , lakini hakuna taarifa
zaidi kuhusu tukio hilo.
Baadhi ya ripoti zinasema kuwa huenda Zeidan amezuiliwa.
Mnamo siku ya Jumanne waziri mkuu Zeidan alitoa
wito kwa Marekani na nchi za Magharibi kukomesha vitendo vya wapiganaji
wenye itikadi kali nchini Libya.
Kwenye mahojiano na BBC, alisema kuwa Libya inatumiwa kama kambi ya kuweka silaha.
Waziri mkuu aliambia BBC kuwa nchi yake inatumia
kama kivukio cha kusafirishia silaha kwenda katika maeneo mengine ya
kanda hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni